Kawaida sisi Wanawake huwa tunanuna pale tunapokoseawa tukitegemea kuwa Jamaa anakereka kwa kuchuniwa na hivyo ama kukuuliza tatizo ni nini ili umpe Risala au straight up agundue kosa alilokufanyia na akuombe Msamaha. Wengine hawajali hata ukiwanunia, wanachukulia ni "mambo ya Wanawake" na Baada ya Muda utakuwa "fine". Wengine hata ukiwaambia kuwa umehisi kuwa amekukosea/umiza hisia zako na hivyo ni vema akuombe radhi bado ataendelea kujitetea, matokeo yake Ugomvi unaibuka. Sasa unakabiliana vipi na Mwenza kama huyu? Kama nilivyogusia kwenye Post iliyopita hapa Malezi ya Mwenza wako yanahusika zaidi kwenye suala la kukubali Kosa na kuomba radhi. Baadhi ya Wanawake wapo hivyo pia lakini tofauti ni kuwa baadhi yetu huwa tunapewa Elimu ya Awali ya Maisha ya Ndoa hivyo hata kama Mama na Baba walijisahau au hawakujali kutupa malezi mema bado tutajifunza Ukubwani ili kuwa tayari kuishi na Mtu Baki(Mume). Makosa ninayoyazungumzia hapa ni yale madogo-madogo na