....kwa maana ya yeye kubadilika/shwa na "Rafiki" zake kama niliyogusia Post iliyopita, ikiwa hukuisoma basi bonyeza hapa. Upo salama lakini?....twenzetu!
Kwanza kabisa usimwambie kuwa umebadilika, lakini akikujia na mambo mapya ambayo awali hakuwa akipenda/fuatlia then hoji kulikoni? mf: tangu lini Mpenzi unatazama Eastenders? Hee siku hizi unafuatilia hiki/kile? hii itamfanya atambue kuwa unaona mabadiliko.
Pili, Jiweke mbali, yaani mbaaaaaali na hao/huyo "Rafiki" unaedhani ana/amembadilisha Mwenza/Mpenzi wako. Usimuulizie, akianza kukupa stori bila kutaja jina la Mhusika, wewe sema tu "tunamzungumzia John"(taja jina la huyo rafikie mpya)? Halafu onyesha kuwa huna "interest" ya kujua zaidi.(hii itafikisha ujumbe na hivyo kuacha stori za huyo mtu/watu).
Tatu, Ataanza kutaka kukutanisha wewe na huyo "Rafiki" kwa kisingizio chochote tu, kuanzia "ametualika kama familia" au "anataka kuja kututembelea ili awaone watoto/apajue Nyumbani". Weka Mguu chini na mtolee Nje kwa upendo na upole kwa kumwambia kuwa Mpenzi/Mume wangu....vyovyote unavyomuita. Ashura ni Rafiki yako, mmekutana Kazini na nafurahi umejenga urafiki na mtu Mahali pa Kazi. Ila ni vema kama ukitenganisha Maisha yako ya Kazini na ya Nyumbani.
Hapa lazma atabisha kwasababu atakuwa tayari kaongea na kumhakikishia "Rafiki" yake kuwa atakwenda na Familia/Mke/Mume wake, sasa ili asimuangushe ni wazi atakubishia na hata kuonyesha Ukali na kukufanya ujisikie kuwa hupendi watu, atasema hakuelewi, atasema umebadilika na mengineyo basi tu kukuuudhi ili umkubali. Usi-panick. Tabasamu na Mwambie haupo Comfy kukutana na Mtu wa Kazini kwake amjue yeye Mumeo/Mkeo/Mpenzi wako huko na sasa amjue Nyumbani pia.
Ongeza kwa kusisitiza (ukiwa firm bila kufoka) kwamba huyo ni Rafiki yake yeye na sio Rafiki wa Familia yenu hivyo basi ni muhimu ya Kazini yabaki huko na ya Nyumbani yabaki Hapa(nyumbani). Kama ni muhimu sana na hutaki kumuangusha rafiki yako, basi nenda mwenyewe. Mimi na Watoto(kama mnao) hatuhusiki na urafiki wako wa Kikazi.
Nne, Mwambie mwenza wako kuwa ni vizuri kutengeneza Marafiki lakini ni vema zaidi ikiwa mtatengeneza marafiki kama Pea nje ya Kazi, kwamba muwe na Marafiki wapya ambao hamkukutana Kazini. kwasababu kuwa na Rafiki anaekujua Kikazi, Kisosho na Kifamilia/Nyumbani ni Hatari na ni Mwanzo wa kutengeneza Adui.
Kumbuka, wapo watu wanatafuta Marafiki ili kujenga Uadui mahali pa Kazi. Utendaji ni Ushindani. Kupata kazi na Kubaki kwenye kazi na hatimaye Kupanda Cheo kunahitaji Ushindani. Ushindani huo unaweza ukawa Mzuri kabisa na ulio-base kwenye utendaji na Bidii yako, lakini pia wapo ambao hupenda njia za Mkato.
Sasa unapoanza Kazi mpya, unakuwa "vulnerable" na hivyo "maadui" huchukua nafasi hiyo ili waje kukumaliza kirahisi huko baadae. Sikutumi kuwa usijenge marafiki kwa kuhofia wao kuwa Maadui baadae, isipokuwa nasema kuwa ni muhimu Rafiki wa kzini wabaki huko na Nyumbani wawe wengine. Ikitokea Kazini kumebuma, angalau Nyumbani kutakuwa Salama....kwamba hamtowavuruga Watoto na hakutakuwa na "Mama mbona hatuendi tena kwa akina Peter"? "Mama naomba kumpigia Simu Antie Rose". Vilevile Adui hatokuwa na lolote alijualo kuhusu Nyumbani kwako na kulitumia ili kukumaliza zaidi.
Nadhamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments