Hello! Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Mambo tunayoambiwa tuyafanye kwenye Ndoa ili tuishi kwa Amani ni mengi mno na yanachukua "utambulisho" wetu......halafu vipi kuhusu Ndoa yenye furaha?
Mambo kama "usilopokea....soma nyakati kwanza ili usimuudhi mwenza wako", hii inakufanya uwe mtu mwingine na sio wewe.....katika hali halisi ni task itakayokukosesha furaha kwasababu utakuwa unaishi kama mtu mwingine na sio wewe.
Unasoma nyakati only kama issue unayotaka kuiwakilisha kwa mwenzio ni ya kubomoa au kujenga Ndoa yenu. Lakini mambo ya kawaida kama vile kutaniana na kuzungumzia watoto hayahitaji "kusoma nyakati".
Kingine ni kusema unavyojisikia baada ya kuvumilia vya kutosha.....ujue wakati wote sisi ni wepesi kuona makosa madogo madogo ya Wenza wetu kuliko kuona yetu(sio rahisi kuona makosa yako).
Na ikitokea Mwenza sio mwepesi kukuambia pale unapokosea basi wewe unadhani kuwa ni kawaida tu na unasonga na maisha.
Siku yakimfika shingoni anakuambia rasmi kuwa "kuna siku nitachoka kuvumilia nitabwaga manyanga".....hapo ndio unaamka na kuanza kutafuta makosa yako.
Sasa siku hizi tunaambiwa tusiwaambie Wenza wetu kuwa "tunakaribia kuchoka kuvumilia" kwasababu hiyo itawaudhi na hivyo kuharibu Amani Ndoani.
Hivi unajua kuwa bila kuwa na furaha Ndoani hakika hukutakuwa na Amani?
Ili kuwa na Ndoa yenye furaha ni vema kila mtu kuwa yeye na sio ku-pretend kuwa mtu mwingine ili usimuudhi Mwenza wako.
Kosa likijitokeza liweke wazi na mlizungumzie na kwapamoja kutaguta namna ya kuliepuka(kosa sio cheating.....cheating haina kuzungumza).
Jinsi siku zinavyokwenda na Ndoani unakuwa too comfortable to the point unapoteza hadhi ya Mpenzi unaanza kuwa Baba/Mama yake. Unaweka vijisheria vya kipuuzi vingi.....usinishike hapa.....usiongee na mimi hivyo....usivae hivi.....my FAV....SIKU HIZI HUNA HESHIMA!
Nani anataka kulala na Baba/Mama yake? Total Kuneng'enuana off put.
Babai.
Comments