Skip to main content

Baba/Mama yao Mzungu.....?

Watu(Wazungu) wanapouliza kama Mumeo/Mkeo ni Mzungu kwasababu watoto ni weusi na sio WEUSIiiiiii tii, unafurahi? Unakwazika?  au unapata (mie)nafasi ya kutoa Elimu kuwa Weusi wetu Waafrika unatofautiana na kwanini?



Nilikwisha wahi gusia kuwa kuna baadhi ya watu Shuleni kwa Babuu wanadhani Baba yake ni Mzungu......nikiwa na Kibibi ambae hana rangi ng'avu sana kama Kaka yake bado watu wanadhani Baba yake ni Mzungu.





Halikadhalika watoto wakiwa na Asali wa Moyo (baba yao)bado wanauliza "is their mother white"?



Inafikia mahali unachoka kutoa Elimu ya tofauti ya Weusi......jamaa wanadhani Waafrika wote tuna rangi moja kwamba wote ni Chocolate au Dark Chocolate.



Ikitokea unakarangi ka Caramel au umepauka zaidi basi wewe ni mixed race(toa macho kwa mshangao)!




Sasa hili ni Jepesi kwa Mimi mkimama wa Kitanzania(sikwaziki kirahisi).....ilimtokea Mkimama mmoja wa USA ayeeee alikasirika mpaka akaamua kwenda public(youtube).....Weusi wa USA wapo verevere demaged na Ubaguzi.




Pamoja na hasira zake bado mtoto sio wake wa kumzaa.....anamtunza tu wakati anasubiri kupatiwa "a home". Imagine angekuwa kamzaa sasa.



Najua Ubaguzi upo UK na hakika Wazungu ni wabaguzi sema wengi inabidi watuchukilie kama tulivyo kutokana na "sheria" dhidi ya Ubaguzi, pia hii ni 2015 sio 1920




Pamoja na kusema hivyo bado wapo baadhi hawajui tofauti yetu sisi weusi kama vile ambavyo wengi wetu(wenu hihihi) hamjui tofauti za Wazungu. Mnadhani Mzungu=Maisha mazuri/mapenzi ya kweli.



Usikute tukitoka kama familia wanadhani Mimi na Asali wa Moyo ni Childminders au tume-adopt.


Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao