Skip to main content

Wanaume na tofauti zao....


Kuna wale wanaodhani kuwa na wewe ni "Feva" hivyo ushukuru Mungu. Aina hii huwa wanategemea uwafanyie kila kitu kuanzia kuwapikia mpaka kutafuta mbinu za kuendeleza "moto" kwenye ndoa yenu.


Unafanya yote hayo na pengine zaidi.....yeye ana-chill tu. Yaani hata ukiumwa hakutengenezei Uji. Inafikia mahali unajiuliza "nafanya yote haya kwa ajili yake, yeye ananifanyia nini?


Pili, Wanajifanya wanaujua Usawa kuliko Feminist (well wanaume pia wanaweza kuwa mafeministi as in wanasaidia kupigania Usawa kwa wote). Lakini sasa kwanini ni wewe tu ndio umnunulie Zawadi ghali na wewe kupata Kadi tu kutoka kwake kwenye ile siku yenu Maalum?


Tatu, Wazee wa Mipango aka wazito.....huyu bwana ana plans lundo halafu nzuri zinazotekerezeka lakini utekerezaji Sufuri. Sasa si unipe mgao mie nikutekerezee? Mpaka nikuombe....Aiii!



Nne, Wadaku.....kila stori ya Mjini anayo yeye....kila mwanajamii wa jamii yake ama anamjua au rafiki yake ni rafiki yake. Anashadadia(bado mnatumia hili neno?) Matatizo ya wenzie na kujadili nini kifanyike ili matatizonyawaishe......wakati matatizo yake yanamshinda.



Tano, Wasambaza Umasikini. Hakupendi na hana mpango na wewe anachotaka ni hizo dakika tatu za Ngono, lakini kutumia Condom ni Mwiko......huyu anaacha mabegu (uchafu)wake popote.....i mean kwa mwanamke yeyote(anapima kama anauwezo wa kuzaa).



Hawa bana anaeza kuivaa Condom halafu katikati ya mchezo akaivua bila wewe kujua.......au....au kama upo nae kwenye uhusiano anajifanya "nimeshindwa kujizuia ujue wewe ni mtamu sana".....mwenyewe unaona siiiifa unatunza Kamimba.



Kimbia(sikutumi ila kama haeleweki inabidi uzuie kabla haijatunga) kachukue kale kakidonge kanaitwaje kaleeee.....night after? Nani anataka "oops baby" Maisha haya?.



Sita, Marafiki Mbele, Familia nyuma......umewahi kusikia msemo wa "familia Daima".....familia kwa maana ya ile unayoianzisha sio kule ulikozaliwa.


Saba, walazimisha Undugu.....usinielewe vibaya lakini kama hamchangii damu pande zote mbili huna undugu.....hao ni Jamaa tu.


Nane, Wakosoaji! Kabla hawajajua kwanini umefanya ulichofanya wanakuja full force na makritisizim yao. Uliza kwanza Mwanaume.


Tisa, wapenda watoto tu sio Mama zao. Well inawezekana kabisa hasa kama mama alikuwa "mapoozeo".....Ujue Ngono kwa wanaume WENGI huwa ni Ngono tu.


Huwa hawaweki emotions na mara zote hawaifanyi kwasababu wanakupenda.  Wanafanya ilinkumaliza haja ya mwili. Rejea namba Tano.


Kumi, niligusia jana. Wanakuwa Baba yako zaidi kuliko Mpenzi....huyu bana kila akikugusa kimapenzi unarudi nyuma na kukumbuka alivyokufokea au alivyokukataza usimshike tako"......wasifu wa Baba huu hapa"....unapoteza hisia.


Kumi na Moja, hawajui kusema ahsante(kushukuru)......hawajui kuomba Msamaha(mpaka u-demand) which inapoteza maana ya Msamaha.

Hii inakufanya  uogope kuwaacha watoto wenu kwa Wakwe.....maana kama baba yao hakufunzwa basics na wazazi wake walipokuwa Vijana....leo wamezeeka wataweza kuwafunza wajukuu?

Kumi na Mbili, watishiaji/wamikwara......"usipobadilika nakuolea mke wa pili" hehehehehe well dear nami nakuletea mume mwenza.....hii ni 2015 sio 1984 pale mama yako alitishiwa hivyo.

Kumi na Nne(13 ni namba ya Mikosi UK).....wanaolazimisha watoto waliowazaa kabla yako.....kipindi ndio anakutaka-taka(anakutongoza) au mpo pamoja......kutwa anachomekeza habari za mwanae "my baby this....my baby that......aaah mwanagu kapata mama mzuri kweli" (yaani wewe).

Unatamani kumwambia "unanipotezea mzuka bana....najua mwanao ni muhimu kwako naomba ibaki hivyo wacha ku-push on me".....as in am not interested.

Aaah sitaki Post iwe ndefu wacha niishie hapa! Ahsante kwa kuchagua blog hii.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao