Habari?
Unajua enzi hizo kuishi Ulaya(ya UK) ilikuwa raha sana na tulikuwa na mahela ya kumwaga.....hata mie nilikuwa tajiri Mwanafunzi.
Unakumbuka enzi zile tulipokuwa summer holiday(kipindi kama hiki) unagoma kurudi kwenu na badala yake unabaki Ulaya kupiga Kazi siku 7 za Wiki ili "kufuga" pesa?
Wakati wa term mtu kutoka Bongo anakuomba senti.....unamwambia nipe wiki nitakurekebishia......unaenda chukua kazi kwa Wakala na unamaliza tatizo la mtu just like upepo.
Fast foward mpaka 2008.....wa Ulaya Mashariki wakaanza kumiminika nankujaza kazi zote za Mawakala tena kwa malipo chee(wanachukua mpaka £3 kwa saa)......sasa mimi Muafrika na yule Mbritish (kiwango cha malipo ni tofauti na wa Ulaya Mashariki)! nikufanyie kazi lwa £3 sijipendi??
Siku hizi ni kama Bongo tu.....kama hujapata bonus kazini kwako basi utabaki na Mshahara ule ule......siku hizi hata zile overtime hazipatikani. Mkurugenzi anachukua extra hours hihihihihi.
Sasa mtu akikuomba msaada na ukamwambia....eh bana life ngumu UK samahani siwezi kukusaidia anakuona unaroho mbaya tu/umebadilika.
Ndio mimi ni Matanzania muhamiaji lakini siwapendi Wahamiaji wa Ulaya Mashariki kwasababu nilizogusia hapo juu. Naiomba Serikali iweke sheria ngumu kwa Wahamiaji wa Ulaya Mashariki.
Hee majuzi hapa tukaletea Mchango wa Ndoa ulioambatana na ujumbe "kwasababu Ndugu tupo wachache UK tumeamua kila Ndugu atoe £500"......kweli? Kweli kabsaaaaa......bila aibu? Nendeni mkaoane Bongo kuna Ndugu kibawooooo.
*Ndugu wa kupanga matofali(sio baba na mama mmoja). Sante kwa kuchagua Blog hii.
Babai.
Comments