Mtu aliehamia Nchi nyingine kwa Kupenda(uamuzi wake binafsi) nae ni "Diaspora" au ni "Migrant" au yote mawili kwa pamoja? kwasababu tunatumia neno "dayaspora" wacha niende nalo ili kurahisi mambo. Wewe umeishi zaidi ya miaka 10 nje ya Tanzania, umejenga Marafiki(ndugu) wapya, umeanzisha Familia(ambayo haina uzoefu na Nyumbani kwa Wazazi/Mzazi mmoja) na kuwekeza kwenye "Property(ies)" na Biashara nyingine. Lakini ukifariki "watu" wanalazimisha uzikwe kwenu(sio kwako kwenye Familia uliyotengeneza ambako ndiko ulikofia) na Marafiki wa Ukubwani. Sio tu ni ubinafsi wa Jamii hiyo "nyumbani" bali pia ni kujipa Majukumu na Gharama ambazo sio zao(hata kama wanachangisha) bila kusahau kuwanyima Watoto na Mkeo/Mmeo Haki ya kutembelea Kaburi lako wanapohitaji kufanya hivyo. Familia yako kutumia Milioni kadhaa kuja "Nyumbani" kila mara wanapotaka kuongea na Mzazi/Mwenza wao ulielala Kaburini ni ghali. Ukiachilia hil