Mtu aliehamia Nchi nyingine kwa Kupenda(uamuzi wake binafsi) nae ni "Diaspora" au ni "Migrant" au yote mawili kwa pamoja? kwasababu tunatumia neno "dayaspora" wacha niende nalo ili kurahisi mambo.
Wewe umeishi zaidi ya miaka 10 nje ya Tanzania, umejenga Marafiki(ndugu) wapya, umeanzisha Familia(ambayo haina uzoefu na Nyumbani kwa Wazazi/Mzazi mmoja) na kuwekeza kwenye "Property(ies)" na Biashara nyingine.
Lakini ukifariki "watu" wanalazimisha uzikwe kwenu(sio kwako kwenye Familia uliyotengeneza ambako ndiko ulikofia) na Marafiki wa Ukubwani.
Sio tu ni ubinafsi wa Jamii hiyo "nyumbani" bali pia ni kujipa Majukumu na Gharama ambazo sio zao(hata kama wanachangisha) bila kusahau kuwanyima Watoto na Mkeo/Mmeo Haki ya kutembelea Kaburi lako wanapohitaji kufanya hivyo.
Familia yako kutumia Milioni kadhaa kuja "Nyumbani" kila mara wanapotaka kuongea na Mzazi/Mwenza wao ulielala Kaburini ni ghali. Ukiachilia hilo mbali hao wanaolazimisha "ukazikwe kwao"...wakisha zika hawatembelei tena Kaburi lako kwasababu wameisha zoea kutokukuona mara kwa mara kwa sababu ulikuwa anaishi mbali.
Binafsi sikuwahi kuona umuhimu wa wapi Mfu anatakiwa kuzikwa, mpaka Kaka yangu alipofariki na Ndugu kutaka azikiwe Nyumbani(Baada ya yeye kuishi nje ya Tz kwa miaka 22 ). Hoja yangu ya "Ni vema azikiwe alikoishi maisha yake ya Ujana karibu na Mkewe na watoto wake" ilipita japo kwa mbinde.
Weka pembeni suala la kusafirisha Maiti kutoka nchi yeyote ile ni ghali(japo unasafirishwa kama Mzigo), kuna suala la Waombolezaji Kula/Kulala mpaka Mwili wako utakapo wasili na pia kule kwako (ulikofia) kuna Maturubai na waombolezaji pia.
Vilevile kuna Gharama za kutunza Mwili, kuuandaa/tengeneza na nauli za Mke/Mume aliebaki na Watoto.
Ni wawache sana wanaweza kumudu gharama hizo za ghafla lakini kwa upande mwingine(tunza, andaa mwili kwa muda mrefu, nauli, Maturubai na kulisha watu huku na kule) ni kujitakia.
Ifike mahali "Dayaspora" waridhike kuzikwa kwenye Nchi wanazoishi ili kurahisisha ukaribu na Familia zao walizoanzisha na sio zile za Wazazi wao(origin).
Familia yako uliyoitengeneza ina Haki ya kuwa karibu nawe hata katika Ufu(ukiwa Kabirini) mara nyingi iwezavyo bila kufikiria Nauli/Usafiri na Hotels.
Nikukumbushe sehemu ndogo ya Umuhimu wa kufunga Ndoa. Kama mmefunga Ndoa, wewe ndio una Haki na Mamlaka ya kuamua Mwenza wako azikiwe wapi, na sio Wazazi/ndugu zake.
Ikiwa unaishi mwenyewe na hivyo kurudi Nyumbani ni Muhimu(huna Familia Ulaya) hakikisha una Bima ya Afya/Maisha(na Mazishi) kwenye Nchi uishiyo, ili kuwapunguzia Mzigo Wazazi wako "Nyumbani".
Nathamini Muda wako, ahsante.
Comments