Skip to main content

Posts

Showing posts with the label diaspora

Diaspora Wives...

...the long suffering ones wa US, UK and Canada nyie wa Scandinavia, Spain, Italy, Germany, etc hamuolewagi...wait, huwa hamuolewi na Waafrika wenzenu na wengi ni Mama wa nyumbani (natania). Dayaspora wives work several  shifts in the cold and spend the  money to support their husband's  business ventures in Africa. Them ones who want something back home, they want to become somebody somewhere kule kwa Motherland.  Mnakubaliana vema tu kuwa mara 4 kwa mwaka yeye atakuwa anaenda Tanzania au Kenya(depends on their origin) na kukaa huko kwa wiki 2 mpaka mwezi "kusimamia" Mradi/Biashara,  hiyo ni kila baada ya miezi 3.                                       picha kutoka gazeti la The Telegraph*? Kwasababu ya yeye kurudi kwao/kwenu mara kwa mara ni wazi kuwa haingizi kipato cha kutosha na hivyo yeye sio breadwinner isipokuwa wewe mkewe. Unajitolea mhanga ukiamini kuwa Mradi ukikamilika utaacha kufanya kazi kwa kiwango ufanyacho na Mumeo kuwa breadwinner, a provider

Dayaspora na Uraia Pacha...

Natumai unamalizia vema Mwezi huu wa 3(na Dayaspora). Suala la Uraia pacha ni zuri sana na lina faida nyingi kwa pande zote Mbili za Watanzania(Ndani na Nje), na Taifa lenyewe kwa ujumla(hasa kwenye Michezo Kimataifa, Uchumi, Afya na Elimu). Uwekezaji? Sio sana kwasababu kama Mtanzania utataka "kupendelewa" au "kupunguziwa" Masharti kutokana na Uraia wa Taifa hilo la Uzawa wako na hivyo Serikali kupoteza Mapato(Visa ya Uwekezaji na gharama nyingine) kutoka kwa Wawekezaji wa Kigeni.  Dayaspora wengi wanadhani kuwa Serikali inakwepa suala la Uraia Pacha kwa sababu ya Wivu, Chuki au Uoga wa "kupitwa" Kimapato, Ujuzi na Uzoefu. Kwaharaka haraka(uvivu wa kufikiri) inawezekana kweli ni Roho ya "kwanini wao", lakini ukiamua kutulia na kwenda ndani, utagundua kuwa  Taifa(Serikali) itapa Hasara zaidi kuliko mnavyorembesha Faida za Uraia Pacha. Hasara za Uraia Pacha zipo nyingi ila mie ninazo Nne tu. Tangu kupata Uraia wa Tanzania ni rahisi(kwa sababu ya M

Dayaspora vs Wazawa "groundini"...

Enzi Watqnzania "waishio" Twita walikuwa wakiwasimanga Diaspora kwa kujifanya wanajua kila kitu, mie nikaandika hii  kaisome tafadhali. Imekua kawaida kwa Wabongo wa Tz na wale wa Nje ya Tz kupishana mara kwa mara, huenda ni kwa Utani uliojificha kwenye yalioujaa Moyo ambayo ni ukweli au kuchangamsha Genge. Kuna wakati huwa naona "point" ya wale wa Bongo kuachwa wajadili na kuishi naisha yao na Siasa zao, lakini wakati huo huo naelewa kwanini Dayaspora wanapata hitaji la kutaka kutoa maoni/mawazo yao kuhusu Bongo kwasababu (wana Miradi, Ndugu na Jamaa...ni Kwao pia) wanaguswa kama unavyoguswa wewe. Kitu kingine ambacho Wabongo wa "Graundini" wanapaswa kujua au kujifunza kukubali kuwa,  "Dayaspora" wana-options tofauti kulingana na Muda gani ameishi huko aliko. Mtaani, Chuoni na Kazini yupo na watu wale wale wanaongea masuala tofauti kuhusu Nchi tofauti ambayo katika hali halisi ha-relate(inategemea kaishi huko nuda gani). Akija Mtandaoni anakutan

"Dayaspora" na Kuzikwa "Nyumbani"...

Mtu aliehamia Nchi nyingine kwa Kupenda(uamuzi wake binafsi) nae ni "Diaspora" au ni  "Migrant" au yote mawili kwa pamoja? kwasababu tunatumia neno "dayaspora" wacha niende nalo ili kurahisi mambo. Wewe umeishi zaidi ya miaka 10 nje ya Tanzania, umejenga Marafiki(ndugu) wapya, umeanzisha Familia(ambayo haina uzoefu na Nyumbani kwa Wazazi/Mzazi mmoja) na kuwekeza kwenye "Property(ies)" na Biashara nyingine.  Lakini ukifariki "watu" wanalazimisha uzikwe kwenu(sio kwako kwenye Familia uliyotengeneza ambako ndiko ulikofia) na Marafiki wa Ukubwani. Sio tu ni ubinafsi wa Jamii hiyo "nyumbani" bali pia ni kujipa Majukumu na Gharama ambazo sio zao(hata kama wanachangisha) bila kusahau kuwanyima Watoto na Mkeo/Mmeo Haki ya kutembelea Kaburi lako wanapohitaji kufanya hivyo. Familia yako kutumia Milioni kadhaa kuja "Nyumbani" kila mara wanapotaka kuongea na Mzazi/Mwenza wao ulielala Kaburini ni ghali. Ukiachilia hil