Natumai unamalizia vema Mwezi huu wa 3(na Dayaspora). Suala la Uraia pacha ni zuri sana na lina faida nyingi kwa pande zote Mbili za Watanzania(Ndani na Nje), na Taifa lenyewe kwa ujumla(hasa kwenye Michezo Kimataifa, Uchumi, Afya na Elimu).
Uwekezaji? Sio sana kwasababu kama Mtanzania utataka "kupendelewa" au "kupunguziwa" Masharti kutokana na Uraia wa Taifa hilo la Uzawa wako na hivyo Serikali kupoteza Mapato(Visa ya Uwekezaji na gharama nyingine) kutoka kwa Wawekezaji wa Kigeni.
Dayaspora wengi wanadhani kuwa Serikali inakwepa suala la Uraia Pacha kwa sababu ya Wivu, Chuki au Uoga wa "kupitwa" Kimapato, Ujuzi na Uzoefu.
Kwaharaka haraka(uvivu wa kufikiri) inawezekana kweli ni Roho ya "kwanini wao", lakini ukiamua kutulia na kwenda ndani, utagundua kuwa Taifa(Serikali) itapa Hasara zaidi kuliko mnavyorembesha Faida za Uraia Pacha.
Hasara za Uraia Pacha zipo nyingi ila mie ninazo Nne tu.
Tangu kupata Uraia wa Tanzania ni rahisi(kwa sababu ya Mfumo mbovu, Umasikini na Rushwa) ni wazi kuwa Nchi itajaa Wageni ambao hawana Asili ya Bongo.
Unakumbuka Wasomali waliokuja na Mahela yao na "kununua Uraia" na vibanda vya Wenyeji pale katikati ya Jiji na Maeneo mengine Dar es Salam na kusimamisha Maghorofa? Angalau tumekuwa na Maghorofa Mengi na wanalipa Kodi(I hope).
Vipi Uwingi wa Watanzania(wa kununua) 2005-8 kutoka Nigeria ili waweze kwenda Nchi Canada? Umekumbuka eeh, pengine ndio umejua leo. Hilo moja.
Pili, Umiliki wa Ardhi na Urahisi wa kuhamisha Maliasili. Kwasababu ya Uwezo wa Kiuchumi wa Watz(wa kununua kutoka Ulaya na Nchi nyingine) itawarahisishia Umiliki wa Ardhi(Mali) ambao ni ngumu/ghali kumiliki huko watokako.
Urahisi wa kununua Ardhi kwa Watz(wasio na Asili) itapelekea "Utumwa" kurudi na pia kuongeza gharama na hivyo Wenyeji kushindwa kumudu Bei ya kumiliki Maeneo kwa ajili ya Vizazi vyao vijavyo.
Tatu, Uhalifu wa Kimataifa, ambao utapelekea Nchi mbili kupishana na hivyo kufarakana hali ambayo itasababisha Ushirikiano mbaya na Nchi nyingine(inategemea Mhalifu kafanya nini au kafanyiwa nini na yupo Nchi gani).
Ufisadi/Ukwepaji wa Kodi, Ikiwa Vigogo wanaiba senti ndogo za Misaada na kwenda kuficha Uswis, unadhani "Watz wa kununua" wanashindwa vipi kufanya hivyo kwenye Benki za Nchi zao Pacha....wakijua wazi kuwa TRA haina nguvu, Mamlaka wala uwezo wa kufanya chochote kwenye Account zao. Nne.
Nakubaliana na Serikali kuwa kwa sasa Tz haipo tayari kuruhusu Uraia Pacha kwa Mtu yeyote ili kuwalinda Wananchi wake na Maliasili zake.
Lakini wakati huo huo ni Muhimu watafute namna ya kuwaongezea Muda wa Uraia Pacha Watoto wa Dayaspora(hawakuomba kuzaliwa Ng'ambo na kupata Utaifa walionao Automatically) kutoka Miaka 18 na kuwa Milele.
Hilo lifanyike kwa Umakini wa hali ya juu kwa kuhakikisha kuwa Wazazi wa Watoto hao(Dayaspora) wana Asili ya Tz ya kweli. Kwa uthibitisho wa kuzaliwa kwa Bibi na Babu wa mzazi wake ambae ana Asili ya Tz....mtajua wenyewe mtafanyaje, ila msikurupuke.
Na wewe Dayaspora, kama nia ni Kuwekeza nyumbani lakini kwasasa haiwezekani na Mapesa yanakuwasha, basi ni vema kuangalia uwezekano wa kupata Uraia wa SA, Rwanda, Kenya, Canada(rahisi kupata Uraia halali kuliko nchi yeyote niliowai kanyaga Duniani) au Nchi nyingine yeyote inayokubali Uraia Pacha.
Kama wewe ni Dayaspora na hutaki kwenda wekeza SA, AUS au Canada sababu ni mbali na nyumbani(hihihihihiiii) basi Olewa/Oa MBongo mwenzio halafu mkubaliane anabaki na Utanzania wake(Achukue Ukazi na sio Uraia wa Nchi uishiyo) ili kurahisisha Uwekezaji Bongo.
Nimejibana na bado imekua ndefu, hata hivyo tufanye 2 in 1.
Tambua nathamini Muda wako.
Ty.
Comments