Enzi Watqnzania "waishio" Twita walikuwa wakiwasimanga Diaspora kwa kujifanya wanajua kila kitu, mie nikaandika hii kaisome tafadhali.
Imekua kawaida kwa Wabongo wa Tz na wale wa Nje ya Tz kupishana mara kwa mara, huenda ni kwa Utani uliojificha kwenye yalioujaa Moyo ambayo ni ukweli au kuchangamsha Genge.
Kuna wakati huwa naona "point" ya wale wa Bongo kuachwa wajadili na kuishi naisha yao na Siasa zao, lakini wakati huo huo naelewa kwanini Dayaspora wanapata hitaji la kutaka kutoa maoni/mawazo yao kuhusu Bongo kwasababu (wana Miradi, Ndugu na Jamaa...ni Kwao pia) wanaguswa kama unavyoguswa wewe.
Kitu kingine ambacho Wabongo wa "Graundini" wanapaswa kujua au kujifunza kukubali kuwa, "Dayaspora" wana-options tofauti kulingana na Muda gani ameishi huko aliko.
Mtaani, Chuoni na Kazini yupo na watu wale wale wanaongea masuala tofauti kuhusu Nchi tofauti ambayo katika hali halisi ha-relate(inategemea kaishi huko nuda gani).
Akija Mtandaoni anakutana na watu wa "Nyumbani" na kuzungumza na Wabongo wenzie "exclusively" na ku-relate nao moja kwa moja kuanzia Maisha ya Utotoni mpaka yale ya Shule/Chuo.
Dayaspora Mpya (chini ya Miaka 5)anakuwa anajichanganya zaidi Mtandaoni kwasababu ya "validation", "attention" ili kupata ile "feel good" na Jamii yake.
Nikupe mfano; Mghaibuni akija anakuonyesha jinsi anavyoishi/lea watoto wake kiTz Ughaibuni, utaonyesha "interest" na kumpa "validation" zaidi kuliko akionyesha hayo kwa Jamii ya Watu anaoishi nao huko(hawatojali how unalea mwanao kwa mujibu wa Makuzi ya kwenu au UN).
Wewe wa "groundini" huna options, Ukiwa online ni yale yale, ukiwa mtaani ni wale wale na ukirudi nyumbani ni wale wale.....huenda hiyo ndio ikawa sababu ya kutokuwaelewa baadhi ya Dayaspora na viherehere vyao kuhusu Maisha ya Bongo wakati wanaishi Nje.
Kosa kubwa la Diaspora(nionavyo mimi) ni kulinganisha Maisha yao ya Ughaibuni na yale ya Tz kitu ambacho sidhani kama ni sahihi, japokuwa baadhi hufanya bila kujua kwa sababu za "upya" wao wa Kuishi Ulaya(popote Nje ya Afrika ni Ulaya si ndio?).
Huenda ikawa kweli Dayaspora Wapya(chini ya Miaka5) ni kama Wapwa kule Twita, kwamba hawana/hawajajenga/zoea Jamii inayowazunguuka hivyo wanategea zaidi kuishi "online" na kuonyesha sehemu kubwa ya Maisha yao Mtandaoni.
Nikuache kwa sasa, ahsante kwa Muda wako.
Comments