Skip to main content

Posts

Showing posts with the label dayaspora

Dayaspora vs Wazawa "groundini"...

Enzi Watqnzania "waishio" Twita walikuwa wakiwasimanga Diaspora kwa kujifanya wanajua kila kitu, mie nikaandika hii  kaisome tafadhali. Imekua kawaida kwa Wabongo wa Tz na wale wa Nje ya Tz kupishana mara kwa mara, huenda ni kwa Utani uliojificha kwenye yalioujaa Moyo ambayo ni ukweli au kuchangamsha Genge. Kuna wakati huwa naona "point" ya wale wa Bongo kuachwa wajadili na kuishi naisha yao na Siasa zao, lakini wakati huo huo naelewa kwanini Dayaspora wanapata hitaji la kutaka kutoa maoni/mawazo yao kuhusu Bongo kwasababu (wana Miradi, Ndugu na Jamaa...ni Kwao pia) wanaguswa kama unavyoguswa wewe. Kitu kingine ambacho Wabongo wa "Graundini" wanapaswa kujua au kujifunza kukubali kuwa,  "Dayaspora" wana-options tofauti kulingana na Muda gani ameishi huko aliko. Mtaani, Chuoni na Kazini yupo na watu wale wale wanaongea masuala tofauti kuhusu Nchi tofauti ambayo katika hali halisi ha-relate(inategemea kaishi huko nuda gani). Akija Mtandaoni anakutan

"Dayaspora" na Kuzikwa "Nyumbani"...

Mtu aliehamia Nchi nyingine kwa Kupenda(uamuzi wake binafsi) nae ni "Diaspora" au ni  "Migrant" au yote mawili kwa pamoja? kwasababu tunatumia neno "dayaspora" wacha niende nalo ili kurahisi mambo. Wewe umeishi zaidi ya miaka 10 nje ya Tanzania, umejenga Marafiki(ndugu) wapya, umeanzisha Familia(ambayo haina uzoefu na Nyumbani kwa Wazazi/Mzazi mmoja) na kuwekeza kwenye "Property(ies)" na Biashara nyingine.  Lakini ukifariki "watu" wanalazimisha uzikwe kwenu(sio kwako kwenye Familia uliyotengeneza ambako ndiko ulikofia) na Marafiki wa Ukubwani. Sio tu ni ubinafsi wa Jamii hiyo "nyumbani" bali pia ni kujipa Majukumu na Gharama ambazo sio zao(hata kama wanachangisha) bila kusahau kuwanyima Watoto na Mkeo/Mmeo Haki ya kutembelea Kaburi lako wanapohitaji kufanya hivyo. Familia yako kutumia Milioni kadhaa kuja "Nyumbani" kila mara wanapotaka kuongea na Mzazi/Mwenza wao ulielala Kaburini ni ghali. Ukiachilia hil