Ndio na Hapana.....hello, jambo kabisa?
Wengi sio wajuaji (wanajua sana)ila nadhani ni wazuri kwenye kufananisha..... ukifananisha system ya UK na Tza kwa mfano hakika uta-sound mjuaji(kumbe ni bongolala tu).
Kingine kinachofanya udhani kuwa wa Ughaibuni wanajifanya wajuaji ni uhuru wa kusema, kwamba kila mtu ana Maoni yake kuhusu kila kitu kinachotokea au anachokisoma na pengine kushuhudia.
Uhuru huo (ahsante nyingi kwa Gugo) unafanya baadhi yetu kuweka maoni yetu kwenye issue yeyote ambayo tunahisi inatugusa.
Nikianza kukupa (maoni yangu) mbinu za kukusanya Kodi (nita-base zaidi na system ya UK ambayo naijua lakini wewe huijui) na kuitumia Kodi hiyo kwenye kuboresha Maisha ya Watanzania waishio maisha Duni hakika utaniona nina Akili kweli na ninafaa kuwa Waziri.
Kumbe katika hali halisi mie ni m-bovu wa Hisabati na Masuala ya Kiuchumi siyajui lakini ni mzuri kwenye kujieleza so nikipata "material" naweza kuyaelezea kwa urahisi na kueleweka bila kutumia "statistics".
Unajua kuna tofauti kati ya Mghaibuni alielelewa kimtaani aka uswahilini na yule aliekulia kwenye mazingira ya Kati(kawaida), pia yule mtoto wa Kigogo(high life) bila kusahau alietoka Kijijini break ya kwanza London(kwa mfano).
Sote tunaishi Ughaibuni maisha tofauti kabisa (inategemea na kilichotuleta)lakini Maoni yetu yanaweza kuwa sawa kwasababu System za Nchi zilizoendelea zinafanana.
Pamoja na kusema hivyo bado sehemu kubwa ya wa Ughaibuni wanajua zaidi kuliko wale ambao hawajawahi kuishi Ughaibuni.
Nadhani kinachosaidia zaidi ni mchanganyiko wa watu wengi wenye "Kacha" zao tofauti ambao unakumbana nao kwenye maisha yako ya kila siku.
Kujifunza au kuwa na uwezo wa kumchukulia kila mtu kama alivyo na kumsikiliza kuhusu Kacha na desturi yake(inategemea anatoka wapi Duniani). Hali hiyo inapanua upeo wako....unajikuta unajua taratibu mbalimbali za Maisha ya watu wengi kutoka Nchi tofauti Duniani.
Nyumbani(Tz) tunajichanganya wenyewe kwa wenyewe na tofauti yetu ni Makabila lakini bado tuna-share baadhi ya Desturi na Tamaduni zetu kulingana na Kabila.
Hata kama kuna Mataifa mengine bado sio kwa kiasi kikubwa kama Ughaibuni. Kuishi Ughaibuni kunamfanya mhusika kujifunza mengi bila yeye kujua(bila kuingia Darasani).
Usipofunzwa na Mamayo(Nyumbani) utafunza na Ulimwengu(Ughaibuni).
Babai.
Comments