Skip to main content

Posts

Showing posts with the label nyumbani

"Dayaspora" na Kuzikwa "Nyumbani"...

Mtu aliehamia Nchi nyingine kwa Kupenda(uamuzi wake binafsi) nae ni "Diaspora" au ni  "Migrant" au yote mawili kwa pamoja? kwasababu tunatumia neno "dayaspora" wacha niende nalo ili kurahisi mambo. Wewe umeishi zaidi ya miaka 10 nje ya Tanzania, umejenga Marafiki(ndugu) wapya, umeanzisha Familia(ambayo haina uzoefu na Nyumbani kwa Wazazi/Mzazi mmoja) na kuwekeza kwenye "Property(ies)" na Biashara nyingine.  Lakini ukifariki "watu" wanalazimisha uzikwe kwenu(sio kwako kwenye Familia uliyotengeneza ambako ndiko ulikofia) na Marafiki wa Ukubwani. Sio tu ni ubinafsi wa Jamii hiyo "nyumbani" bali pia ni kujipa Majukumu na Gharama ambazo sio zao(hata kama wanachangisha) bila kusahau kuwanyima Watoto na Mkeo/Mmeo Haki ya kutembelea Kaburi lako wanapohitaji kufanya hivyo. Familia yako kutumia Milioni kadhaa kuja "Nyumbani" kila mara wanapotaka kuongea na Mzazi/Mwenza wao ulielala Kaburini ni ghali. Ukiachilia hil

Ni kweli wa Ughaibuni wajuaji....

Ndio na Hapana.....hello, jambo kabisa? Wengi sio wajuaji (wanajua sana)ila nadhani ni wazuri kwenye kufananisha..... ukifananisha system ya UK na Tza kwa mfano hakika uta-sound mjuaji(kumbe ni bongolala tu). Kingine kinachofanya udhani kuwa wa Ughaibuni wanajifanya wajuaji ni uhuru wa kusema, kwamba kila mtu ana Maoni yake kuhusu kila kitu kinachotokea au anachokisoma na pengine kushuhudia. Uhuru huo (ahsante nyingi kwa Gugo) unafanya baadhi yetu kuweka maoni yetu  kwenye issue yeyote ambayo tunahisi inatugusa. Nikianza kukupa (maoni yangu) mbinu za kukusanya Kodi (nita-base zaidi na system ya UK ambayo naijua lakini wewe huijui) na kuitumia Kodi hiyo kwenye kuboresha Maisha ya Watanzania waishio maisha Duni hakika utaniona nina Akili kweli na ninafaa kuwa Waziri. Kumbe katika hali halisi mie ni m-bovu wa Hisabati na Masuala ya Kiuchumi siyajui lakini ni mzuri kwenye kujieleza so nikipata "material" naweza kuyaelezea kwa urahisi na kueleweka bila kutumia "stat