Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mchango

UK ya leo sio ile ya 1998-2006

Habari? Unajua enzi hizo kuishi Ulaya(ya UK) ilikuwa raha sana na tulikuwa na mahela ya kumwaga.....hata mie nilikuwa tajiri Mwanafunzi. Unakumbuka enzi zile tulipokuwa summer holiday(kipindi kama hiki) unagoma kurudi kwenu na badala yake unabaki Ulaya kupiga Kazi siku 7 za Wiki ili "kufuga" pesa? Wakati wa term mtu kutoka Bongo anakuomba senti.....unamwambia nipe wiki nitakurekebishia......unaenda chukua kazi kwa Wakala na unamaliza tatizo la mtu just like upepo. Fast foward mpaka 2008.....wa Ulaya Mashariki wakaanza kumiminika nankujaza kazi zote za Mawakala tena kwa malipo chee(wanachukua mpaka £3 kwa saa)......sasa mimi Muafrika na yule Mbritish (kiwango cha malipo ni tofauti na wa Ulaya Mashariki)! nikufanyie kazi lwa £3 sijipendi?? Siku hizi ni kama Bongo tu.....kama hujapata bonus kazini kwako basi utabaki na Mshahara ule ule......siku hizi hata zile overtime hazipatikani. Mkurugenzi anachukua extra hours hihihihihi. Sasa mtu akikuomba msaada na  ukamwambia....e