Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mpenzi

Wanaume hawajui kunung'unika/kukaa na Kinyongo....

....Sosho Midia si imewabadilisha? Hakika bado wapo hivyo ila namna wafanyavyo ni tofauti na walivyokuwa wakifanya kabla ya Sosho Midia(nionavyo mimi). Unakumbuka ulipokuwa mdogo(au ni mimi tu), Baba yako akisikia jambo kutoka kwa Mwanaume mwenzie halizungumzii ila anakwenda kwa huyo Mtu na kuzichapa/kumkung'uka Magumi? well Baba yangu alikuwa mtu Mwema na Mtu wa watu lakini alikuwa Ngumi Mkononi, anakutandika halafu yanaisha. sasa hii ndio "Wanaume hawakai na Kingongo" niijuayo mie. Niliendelea kuona hiyo  kwa Kaka zangu na rafiki zao pia na hivyo kuweka Sementi kwenye hilo. Siku hizi Waanaume, wanaanika mambo ya wenzao nje (mitandaoni)ikiwa wamekorofishana, kwamba mmoja akiudhiwa/kasirishwa na mwenzie basi Jamaa wa Shosho Midia wote watajua. Kwa sisi Wanawake ambao hufikiria baada ya action(sio kabla) na kisha kuomba msamaha baada ya kuharibu ni Kawaida(ilizoeleka hivyo), lakini sio kwa Wanaume. Sio kwamba  nasikitika kuwa Wanaume wamebadilika na wala s

Sababu Kuu ya Kumchukia Ex wake...

.....wengi hudhani kuwa ni Wivu au Hofu kwamba Mwanaume anaweza kurudi alikotoka au kukuacha kama alivyomuacha yule ila tofauti ni kuwa anakwenda kwa Ex wake sio Mwanamke mpya. Yote ni  sababu common lakini ile kuu ambayo wanawake wengi hutusumbua na hata kujenga dislike(nikisema hate inakuwa too strong) huenda ni hii hapa chini. Umewahi kutaka kumjua kama Mpenzi wako ana type? na pengine kwenda ndani na kutaka kumuona Ex wa Mpenzi wako kabla yako na hata kutaka kukutana nae? sio ili muwe marafiki bali ni kutaka kuona kama alikuwa Hot au Not....(hihihihihihi). Ikiwa Mpenzi wako ana type na aliempitia kabla yako alikuwa Hot basi unafurahi kuwa na wewe ni hot (pengine wala sio that hot) na kwabahati mbaya kama ex alikuwa Not basi hapo ndio hasira huja. Kila ukimfikiria/kumbuka yule Ex alivyo unamchukia vibaya sana hehehehehe huku unajisemea "am not that ugly" na kujiuliza "am I that ugly?". Yaani sio kwamba unachukia alivyo (kuwa ugly is okay but....) ba

Chunga Ulimi usimuudhi Mpenzi....

Hello! Ahsante kwa kuichagua Blog hii. Mambo tunayoambiwa tuyafanye kwenye Ndoa ili tuishi kwa Amani ni mengi mno na yanachukua "utambulisho" wetu......halafu vipi kuhusu Ndoa yenye furaha? Mambo kama "usilopokea....soma nyakati kwanza ili usimuudhi mwenza wako", hii inakufanya uwe mtu mwingine na sio wewe.....katika hali halisi ni task itakayokukosesha furaha kwasababu utakuwa unaishi kama mtu mwingine na sio wewe. Unasoma nyakati only kama issue unayotaka kuiwakilisha kwa mwenzio ni ya kubomoa au kujenga Ndoa yenu. Lakini mambo ya kawaida kama vile kutaniana na kuzungumzia watoto hayahitaji "kusoma nyakati". Kingine ni kusema unavyojisikia baada ya kuvumilia vya kutosha.....ujue wakati wote sisi ni wepesi kuona makosa  madogo madogo ya Wenza wetu kuliko kuona yetu(sio rahisi kuona makosa yako). Na ikitokea Mwenza sio mwepesi kukuambia pale unapokosea basi wewe unadhani kuwa ni kawaida tu na unasonga na maisha. Siku yakimfika shingoni anakuambia ras