...Mara nyingi watu husema au kuamini kuwa Mtu anapopata Pesa au Kazi mpya inayolipa Vizuri kuliko kazi yake ya Awali huwa anabadilika(nadhani niliwahi kuzungumzia kwanini watu huwa hivyo mwaka jana/juzi). Habari? natumai Uumzima wa Afya. Nirahisi kutodhani kuwa Mtu Mzima hawezi kuwa "influenced" na Mtu au Watu wapya wanaomzunguuka....kwasababu amepita Umri wa miaka 30...lakini kihalisia bado wapo Watu Wazima ambao wamekua Miili tu na Namba zimeongezeka lakini Akili zao bado ni za Kitoto. Bado wanapata hitaji la kutaka kufanana, ku-fit in, kuwa kama yule/huyu,kukubalika n.k. Inasemekana hali hiyo hutokana na Ukosefu fulani wa "attention" kutoka kwa Walezi/Wazazi kipindi ambacho Mhusika alikuwa chini ya Miaka 10. Kumbuka matokeo ya Malezi tuliyopata kutoka kwa Wazazi/Walezi wetu huwa yanaathiri maamuzi (mabaya/mazuri) na Maisha yetu ukubwani. Mtu anahitaji kitu kidogo tu ku-triger alichokosa Utotoni. Achana na hili. Sasa kwa baadhi mabadiliko huwa Waz