Inawezekana Ndugu zako wanaokufuata au uliowakuta(inategemea umezaliwa wa ngapi) sio Damu moja kwamba baba na mama yenu ni mmoja. Umewahi kujiuliza kwanini mtu anaendelea kuzaa na mume/mke ambae anamtenda(tereza nje)? au Utakuta Ndoa inamatatizo lakini wanazaa tu kila mwaka....haikuhusu lakini kama Binaadam kiasilia hatuishi Kudadisi na Kujaji.
Kiasili Watoto tunadhania kuwa Mama zetu ni "Malaika" lakini bwana mwanamke akiamua kushenzika anakuwa Mshenzi zaidi ya Shetwani, tofauti ni kwamba Wanawake ni wazuri kwenye kuficha siri zao. Akitaka usijue Baba yako ni nani basi hutokaa umjue......akikuaminisha kuwa fulani ni Baba yako basi itakuwa hivyo(ukidai DNA unapewa Radhi hihihihihi).
Mtoto wa Kwanza:
Binti yupo na anaempenda lakini Wazazi hawamtaki Jamaa aoe.....wanataka aolewe na mtu wao. Binti anaolewa na mimba yake bila muoaji kujua. Pia Binti anaweza kuwa anaendelea na ampendae ili azae nae batoto atakaowapenda kama baba yao, kuliko kuzaa na limtu alililochaguliwa na Wazazi wake.
Au binti alikuwa mapepe na matokeo yake hajui Mimba ilisababishwa na nani hivyo anatoa taharifa kwa yule ambae anajua atafaidika kwa namna moja au nyingine.....jamaa akikubali ndio anakuwa baba mtoto.
Pia kuna Jadi za Makabila fulani (unayajua) Baba anamfungua Binti yake kabla ya Mumewe, so akishika Mimba anamzaa Mdogo wake huku Mume mtu anajua yeye ni Dume la Nguvu....kagusa tu kitu na Box, kumbe analea Shemeji.
Mtoto wa Kati:
Baada ya watoto kadhaa mama anaamua kupumzika, anaanza kufurahia maisha kama mwanamke. Majamaa wanaanza kutoa attetion ambazo mumewe hazitoi(Mume anamuona Mkewe mama wa watoto wake na sio Mpenzi tena).....mama anajiona "kumbe bado wamo". Anatereza.....mara oops baby! Mnakaribisha mtoto mpya kwenye familia yenu bila kuhoji.
Mtoto wa Mwisho(hasa kama mpo zaidi ya 4):
Mara nyingi Mtoto huyu huwa wa Hasira au kulipiza Kisasi baada ya kugundua kuwa Mumeo alizaaga kabla hamjakutana na hakukuambia au umegundua kuwa aliterezaga sometime Kitambo, kwa hasira unaamua kuneng'enuka Nje.
Utu uzima unaanza kubisha Hodi, uhusiano unaanza kuwa na changamoto zilizo nje ya Uwezo wa Kibinaadamu(matatizo ya kiafya)....Mwanamke anahisi kavumilia vya kutosha na sasa anabwaga manyanga, lakini hataki uteseke hivyo anaendelea kuwa Ndoani lakini Mengi anafanya huko nje. Mara majikuta mnatarajia mtoto, bila kuhoji unajiona Dume la mbegu.
Usitumie maelezo haya ukijifanya Mtaalamu, ni maoni yangu Binafsi kuhusu nafasi hizo za kuzaliwa. Naheshimu na kuthamini muda wako, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments