Umekuwa na mama yako kwa Miezi 9 mpaka 11 kama ulikuwa na bahati, wengine ni miezi 6 na wengine karibu Mwaka(Miezi 12).
Ni mtu pekee unaemfahamu, na unahisi kuwa upo salama na unapendwa, sababu Mtu huyu sio tu amehatarisha maisha yake ili kukubeba na kukuleta Duniani. Mtu huyu ataendelea "kuteseka" sababu unataka ule x4 usiku wa manane, ataendelea kukupenda, kukulinda, kukufunza na kukujali.
Hayo yote hutokea kwa Miezi 3 ya mwanzo, baada ya hapo unamuona mtu huyo Nusu siku, kila unapoachwa unalia sana. Siku zinavyozidi kwenda ukaribu wako na mtu huyo unapungua na kilio chako kinapungua.
Kitendo cha Mtu huyo ambae sasa unamtambua kama Mama(au Anty, Dada wa Kazi ndio Mama yako) kukutelekeza/kukuacha huwa kinaumiza sana.
Sasa umekua na unajitegemea kwenye mambo mengi kama vile kucheza peke yako, kujivisha viatu/nguo nk. Lakini bado ni Mtoto na bado unamuhitaji Mama yako.
Jana la leo Mama amekua nyumbani siku zima, unahisi furaha, upendo na kujaaliwa.....Mama anaamua kutaka kutoka kidogo, anaanga, wewe unaanza kumlilia.
Mama anasema "nenda kavae Viatu twende"...unatoka mbio kuwahi Viatu...ile umefika alipokuwa Mama anakusubiri, hayupo. Kakuacha/kakutelekeza na hujui kaenda wapi. Unauliza mama yuko wapi? Wanakuambia hawajui ila atarudi muda sio mrefu. Unaendelea kulia na kubeba Huzuni, unakosa raha kwa muda fulani. Hiyo itabaki na wewe maisha yako yote.
Utaitumia kama utani kuficha maumivu/lazimisha kicheko, lakini ukitulia na kutafakari unaumia na kujiuliza "sijui kwanini mama alikuwa ananiacha" (unarudi kwenye maumivu yako ktk umri ule).
Ofcoz haitakuathiri, watoto wa Kiafrika ni "tough" sio kama Wakizungu(by the path baadhi ya Watoto wa Kizungu hufanyiwa hivyo pia).
Nikukumbushe umethirika vipi na kutelekezwa/achwa na Mama yako...
1-Hujawahi kudumu kwenye Mahusino na mtu(Rafiki/Mpenzi) kwa muda mrefu kwasabu unamuhitaji kupitiliza kiasi kwamba anahisi unamnyima uhuru.
2-Mara kwa Mara unakuwa na hitaji la kuhakikishiwa kuwa Mpenzi hawezi kukuacha.
3- Unashindwa kuwa na mahusiano na mtu mmoja sababu unaogopa ukiachwa na mmoja hutokuwa na "back up".
4-Unaogopa kuwa na mahusiano ya "kudumu" aka muda mrefu aka Ndoa sababu "bora kuwa single kuliko kuachwa/telekezwa".
5-Unaamini kuwa karibu/farikiana na watu mbali mbali ni utajiri, kwamba bila kuwa karibu na watu huwezi kufika popote. Yaani huwezi kufanikisha jambo mpaka uwe karibu na watu kadhaa.
Kidokezo: Kufahamiana na watu ni muhimu, lakini kuwa nao karibu/rafikiana nao sio muhimu.
6-Huoni shida kuacha mtoto/watoto wako na mtu mwingine kwa zaidi ya Masaa 24.
7-Ukiachwa na rafiki/Mpenzi huwa unaumia/lia sana na kwa muda mrefu.
8-Usipojuliwa hali/rudishiwa mawasiliano na Mpenzi unaanza kuhisi kuachwa/telekezwa.
Nikirudi nitabaki hapa kwenye kuachwa/telekezwa kwenye ile "Mama yangu alikua mwema kweli, aliacha kuninyonyesha akanyonyesha mtoto wa mdogo wake"
Usikose.
Comments