Skip to main content

Posts

Showing posts with the label secondary

Siku ya kwanza Kidatoni...Miaka 20 tangu Secondary!

Mwaka huu November inatimia Miaka 20, sasa sio mbaya kama nikiweka kumbukumbu zangu za safari yangu ya Shule kuanzia Msingi mpaka Secondari(intro hiyo hihihihi). Siku ya kwanza naingia kama Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza ili kuwa ngumu maana hakukuwa na mtu nilietoka nae Msingi. Wengi walikuwa wanajigawa kwa makundi kwasababu wanajuana kwa kutoka shule moja ya msingi ama shule zao zilikuwa jirani. Kulikuwa na Wanafunzi kibao kutoka Mlimani Shule ya Msingi, Olympio na Upanga(wajuajiii, mabishoo, Kiingereza kingii). Ikabidi nitafute namna ya kujiunga nao, maana kati yao watakuwa na mimi Darasa moja.....nikaanza kutumia Tiketi ya Kuiba (naongea Kiingereza kwa Nyimbo hihihihihi). Nilikuwa najua nyimbo nyingi ahsante  "Double Compact something Cassete Music system".....unaweka Compact yako halafu unasimamisha ili kuandika mstari wa Wimbo husika. Nilikuwa na "book" full of nyimbo za RnB. Baba(Mungu amrehemu) alikuwa anatununulia hizo eti tujifunze Kiinger