Skip to main content

Posts

Showing posts with the label watanzania

Kuzuia Mimba au Kupoteza Hamu?

Habari ya sasa! Utasema hee Dinah mbona umeshupalia Topic hizi? Well....ninachoandika hakitobadilisha Maisha ya watu na kuwa Bora zaidi ya yalivyo sasa, lakini naweza kusaidia mtu mmoja kuelewa kwa kiasi kidogo....yule ambae ame-google "kupoteza hamu" kwa mwanamke si eti! Kuna ulalamishi kuwa Dawa za kuzia Mimba(pamoja na matatizo mengine kwa baadhi) husababisha Mwanamke kupoteza hali ya kutaka/tamani Ngono. Hakuma chunguzi ambayo ina-support hili ila Wanawake wengi hulalamikia kuwa Hamu hupungua au hutoweka kabisa mara tu baada ya kuanza kutumia Njia za kuzuia mimba Zenye Homono(hata zisizo na Homono huingilia "hamu" ya mwanamke"). Do I look like I am busy? Ukweli ni kwamba kama hali ya kutaka  Ngono ilikuwa juu au chini basi haitobadilika......isipokuwa utaratibu wa Mwili wako ndio utabadilika na hivyo wewe Mkimama kulazimika kuanza kujifunza upya(wengi huwa hawalijui hili) namna mwili wako unafanya kazi. Tena sio Dawa za kuzuia m

Wale wasema "Watanzania" Wavivu/Wazembe/Waoga...

Binafsi naamini kuwa sio sahihi kumuita mtu majina ambayo unauhakika ukiitwa wewe hutofurahia iwe ni kweli upo hivyo au la! Mfano unapomuita Mwenzio Malaya unapaswa kuwa na Uhakika kuwa  Baba ni Baba yako kweli (una DNA bila rushwa). Utamponda huyu hajitumi au Utaiponda Ofisi yake? Sasa kwa sababu tu wewe umezaliwa au kubahatika kuwa na shughuli ya kufanya huna haki ya kuwalaumu na kuwaita majina mabaya kama vile Tegemezi, wanapenda kuomba-omba Wavivu, Wazembe, Waoga, Masikini wa Fikra n.k. Pia wewe wa Ughaibuni, kwavile tu wewe unaishi huko ulipo na kuona Maisha ya baadhi ya "wenye Nchi" mazuri na ukapendezwa na labda utaratibu wa Serikali na kudhani Utaratibu huo umewekwa na "wananchi" hao kwa sababu sio Wavivu/Wazembe au majina yeyote machafu unayowaita Watanzania wenzako basi tambua kuwa unakosea. Kabla ya kuanza kumlaumu na kumshutumu Mtanzania  mwenzio kuwa matizo yake yanasababishwa na yeye kuwa mvivu au kutopenda kujituma au kufanya kazi k

Wale akina bila "mimi" usingekuwa hapo!

Unawajua? Kwanza haujambo? Anhsante sana kwa kuichagua Blog hii. Kwa sie wa Ughaibuni (tuishio nje ya Tanzania)au wale tulioitwa Mjini kusoma au kufanya Kazi pia sisi wa Mtaani tuliamua kujaribu Fani na tukaipatia na tumefanikiwa kimtindo ndio huwa tunabeba hili limzigo. Sawa pengine bila wewe kweli asingekuwa hapo lakini ulifanyanini hasa kwenye mafanikio yake aliyonayo hivi sasa......zaidi ya kuwa njia tu ya yeye kufika hapo na actually ukajaribu kuharibu bila mafanikio? Kwa kawaida sisi wa Ughaibuni tukikaa sawa huwa tunapenda kusaidia wengine waje kujaribu maisha huku. Wanafikia kwako na unawasaidia kutafuta Kazi  na baada ya hapo nauli kwa miezi kadhaa halafu wanaanza kujitegemea. Kutokana na Ughali wa Maisha Ughaibuni well UK + "kikacha" unapaswa kuchangia sehemu ya Bills.....hakuna cha bure na hakuna "nakaa kwa Anti hapa" lipa bill dadaaa au nakutimua.....hapa sio Tanzania. Anyway.....maisha yanakuwa magumu kwa upande wako so unaongeza bidii kwenye kus