Habari ya sasa!
Utasema hee Dinah mbona umeshupalia Topic hizi? Well....ninachoandika hakitobadilisha Maisha ya watu na kuwa Bora zaidi ya yalivyo sasa, lakini naweza kusaidia mtu mmoja kuelewa kwa kiasi kidogo....yule ambae ame-google "kupoteza hamu" kwa mwanamke si eti!
Kuna ulalamishi kuwa Dawa za kuzia Mimba(pamoja na matatizo mengine kwa baadhi) husababisha Mwanamke kupoteza hali ya kutaka/tamani Ngono. Hakuma chunguzi ambayo ina-support hili ila Wanawake wengi hulalamikia kuwa Hamu hupungua au hutoweka kabisa mara tu baada ya kuanza kutumia Njia za kuzuia mimba Zenye Homono(hata zisizo na Homono huingilia "hamu" ya mwanamke").
Do I look like I am busy? |
Ukweli ni kwamba kama hali ya kutaka Ngono ilikuwa juu au chini basi haitobadilika......isipokuwa utaratibu wa Mwili wako ndio utabadilika na hivyo wewe Mkimama kulazimika kuanza kujifunza upya(wengi huwa hawalijui hili) namna mwili wako unafanya kazi. Tena sio Dawa za kuzuia mimba tu ndio zinasababisha hili, bali pia kuwa Mama(Kuzaa kunabadilisha Mwili na Akili).
Unapoongeza Homono ambazo zinaenda kuingilia utaratibu wa Mayai yako ili usishike Mimba ni wazi ile siku ya Kipevuka hutojisikia Nyege sana kama ilivyokuwa awali kabla hujaanza kutumia Dawa za kuzuia Mimba. Nia na madhumuni ya Dawa hizo ni kuzuia Uwezekano wako wa kushika Mimba.
Hivyo Yai linapokuwa "tayari" Dawa za kuzuia Mimba (aina ya Homono) ndio hufanya kazi ya ziada kuzuia na hivyo kukamata (shika/teketeza) zile "sex homono" ambazo hujitokeza kipindi hiki na hivyo kukufanya utake Ngono na kutoa Ute laini ili Mbegu zisafiri kwa "amani" na hivyo kushika Mimba.(Dhumuni la Ngono ni Mimba/Kuzaliana siunajua?)
Hivyo Yai linapokuwa "tayari" Dawa za kuzuia Mimba (aina ya Homono) ndio hufanya kazi ya ziada kuzuia na hivyo kukamata (shika/teketeza) zile "sex homono" ambazo hujitokeza kipindi hiki na hivyo kukufanya utake Ngono na kutoa Ute laini ili Mbegu zisafiri kwa "amani" na hivyo kushika Mimba.(Dhumuni la Ngono ni Mimba/Kuzaliana siunajua?)
Nimekuchanganya? Tuna Homono zaidi ya Moja lakini sasa kwa vile Mie sio Msayansi siwezi kuelezea Kisayansi na hivyo nimejaribu kuelezea kibinaadamu vile ninavyoelewa mimi ili nisikuache.
Nitajirudishiaje "Hamu" sasa?
Unahitaji uelewa na Ushirikiano wa Mumeo/Mpenzi wako(rejea topic Umuhimu wa Furaha ya Mke) pia tambua Mabadiliko na kurekebisha mambo kiakili(jifunze upya kona zako za Utamu/raha) na kimwili(kula kiafya, fanya mazoezi, jipende)....umewahi kujiremba (paka vipodozi) na ukafikia kwenye kupaka Lipstic/Lipgloss ukahisi hamu ya Kuneng'enuka(au ni mie tu? Najitamani hihihihihihi).
Anyway kabla hujakimbilia kukubali kuwa umepoteza Hamu, jaribu kubadilisha utaratibu wa maisha yako ya kila siku (kama nilivyogusia hapo juu) na kufanya jambo ambalo unaamini na kujua kuwa unalipenda na unalifurahia. Unapofurahia siku yako na kupata muda wako peke yako kama "mwanamke" hata kama ni Nusu hakika siku yako itakuwa Njema sana na akili yako itatulia na hivyo kupata muda wa kufikiria mambo ya kufanya na Mumeo kama wapenzi. Unapokuwa na huzuni au hasira/mawazo/hofu siku itakuwa mbaya na hakika hutotaka/tamani kufanya Mapenzi au kuwa karibu na Asali wa Moyo wako.
Kama siku imekuwa na Mishughuliko mingi kama Mama basi jaribu kutulia na kufanya yanayohitajika kufanyika.....kamwe usijipe presha ya kuwahi kumaliza ili kupata muda wako na hivyo kumfurahisha Mumeo....kumbuka Wewe kwanza, watoto halafu ndio Baba yao. Usiwafuate wale Mume wangu kwanza, Kids halafu ndio wao...(hawajui Thamani yao).
Ukipata muda(watoto wakilala), jipatie Dakika chache za kucheza na mwili wako ili ujue wapi panafanya nini na wapi hapako kama enzi kabla hujazaa. Mfano mie.....mmh itakuwa Too much Info....achana na hili.
Ukishajijua inakuwa rahisi kumuongoza Mpenzio/Mumeo na hivyo yeye kuachana na ile Kanuni ya "paji, midomo...shingo....matiti...kiuno...nyuma yabmagoti...ingia kati".Baada ya Kuzaa mwili wa mwanamke hubadilika na kilichokuwa kinamhemesha enzi.....sasa kinaweza m-put off.
Na ninyi wanawake mnaoshupaa kuwasukumia Wanawake wenzenu Mpira wa "Wanawake ni kosa letu"....."Wanawake tunajitakia wenyewe"...."Wanawake hatujitumi". Mnapaswa kujifunza namna mwili wa Mwanamke unafanya kazi na wakati unajifunza tambua kuwa Wanawake tunatofautiana na hivyo mabadiliko unayokabiliana nayo wewe mwingine hana. Tuanze kujiheshimu na kutumia Muda zaidi ili kujijua badala ya kulaumiana hasa linapokuja suala la Ngono na Mahusiano baada ya Kuzaa.
Mwanamke haitaji Mwanaume kufika Kileleni(kama anaujua mwili wake), lakini ili afike Kileleni akiwa na Mwanaume.....atahitaji Mapenzi na ushirikiano wa Mwanaume kimwili na kiakili. The moment mwanamke ana mawazo(akili haijatulia) hakutakuwa na Kilele wala kutaka/kufurahia Tendo.
Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments