....wengi huchukulia suala hili juu juu tu, labda hushindwa kuelewa kwasababu Jamii (ikiongozwa na wanawake wenyewe) huwa hailizungumzii sana kama wazungumziavyo Furaha ya Mume. Furaha ni hitaji la wote lakini nadhani kwa mwanamke ni muhimu zaidi kwasababu bila furaha kwake ni wazi watoto na baba mtu hatokuwa na furaha.
Pia furaha kwa mwanamke inahusika sana kwenye masuala ya kufanya mapenzi.....kama mwanamke hana furaha ni ama hakutakuwa na Tendo au Tendo halitokuwa la kufurahia na badala yake litakuwa ni la kumaliza haja tu kwa Mwanaume(maliza nilale arrg hihihihi).
Wanaume wachache ambao wameshuhudia baba zao wakihakikisha Mama zao wanafuraha mara zote iwezekenavyo, hujitahidi na kuwa hivyo au zaidi kwa wake zao. Hawa hujua namna ya kujali na kuheshimu hisia za mwanamke.
Kwabahati mbaya sehemu kubwa ya Wanaume wamelelewa kwenye Mazingira ya kumuona Mama ni mtu mmoja mvumilivu, mpole na muelevu.....wakati Baba Mkali na Bingwa wa kudharau. Kwamba Mama anapochoshwa na labda maudhi ya Baba na hivyo kuweka hisia zake wazi kwa "ukali".....baba hupata hasira kwanini "mwanamke" amwambie nini cha kufanya....yeye mwanaume na hivyo kuamua kukaa kimya(kumdharau Mkewe) ili yaishe.
Kwasababu najua akimjibu mkewe ni wazi Ugomvi utakuwa Mkubwa kwa maana Baba hato-back down na huenda akaishia Kumpiga Mama....ili kuepusha hilo Baba anajifanya anamsikiliza Mkewe(mama) lakini ukweli ni kuwa hakuna kinachoingia akilini na hakuna atakachofanyia kazi.
Sasa kwa Kijana aliekulia kwenye Mazingira kama hayo(kama nilivyogusia hapo juu) inakuwa ngumu kujua umuhimu wa furaha ya Mmwanamke kwenye Uhusiano wao. Furaha ya "mke" itakuwa na maana nyingine kabisa ambayo mimi na wewe(wanawake kama wanawake tunavyoifahamu).
Kwasisi Wanawake baadhi hukua kwenye Mzingira kama hayo pia lakini tofauti ni kuwa pembeni huwa tunafunzwa namna Mwanamke anapaswa kuwa "treated" na namna gani Mwanaume anapaswa kuwa "treated". Wanaotoa mafunzo huwa ni Watu wazima ambao tayari wamepita kwenye maisha hayo na husisitiza kuwa Waume zao hakuwa hivyo lakini hawakuwa na jinsi kutokana na Jamii ilivyokuwa (kipindi hicho cha nyuma)alipaswa kuolewa kwa wakati ule ambapo aliolewa(hakuwa na option).
Sasa kutokana na kukosa Option, inakuwa kama vile wanajutia na hawataki sisi Wanawake wasasa(tunaofundwa) kuishi maisha walioishi wao.....kudharauliwa, kutosikilizwa, furaha zao kutotiliwa maanani n.k.
Je utamfurahishaje Mwanamke(Mke)?
Inategemea na Mwanamke husika lakini kuna yale ya Jumla ambayo kila mwanamke anahitaji ili kuwa na furaha na hivyo kuwa na Ndoa/Uhusiano mzuri:-
-Msikilize(najua tunaongea sana) lakini ni muhimu kuonyesha unamsikiliza na kumuelewa.
-Mshukuru(sio kwa kufanya Mapenzi) bali kwa lolote ambalo anakufanyia nje ya Kitanda, hata kama ni kidogo kama kukuletea Chai au kukutoa tongotongo.
-Muulize kabla ya kumkosoa(wewe sio Baba yake, hajifunzi kutoka kwako) hivyo ni vema kujua kwanini jambo limefanyika badala ya kukimbilia kumkosoa.
-Zika habari za Ex.....hakikisha huleti habari ambazo unajua zitasumbua akili yake(wale Funs wa kuzungumzia past lives zao kila Mgeni anapowatembelea au kila mnapokutana na watu wapya). Wote mna Past, kwanini udhani yako ni muhimu sana kujulikana kwa kila mtu?!!
-Hakikisha unajua tofauti kati ya Wajibu na Mapenzi, yupo na wewe kwasababu anakupenda......kukupenda sio Wajibu.
-Msaidie kwenye Malezi ya watoto(kama mmejaaliwa kuwa nao), watoto wenu ni Wajibu wenu kama Baba na Mama, sio Wajibu wa Mama pekee.
-Mnunulie Zawadi once in a while hata kama ana kazi na mshahara Mkubwa kuliko wako.
Hey! Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments