Mambo!
Ijumaa Mpya(ya Kwanza Mwezi huu) na Maalum kabisa kwani ni Wiki ya Kwanza tangu kuanza kwa Mitihani ya Kumaliza Kidato cha Nne Tanzania, na ndio Mwanzo wa Mwisho wa Series hii(inaonekana kupedwa/somwa zaidi), inapendeza!
Utakuwa unajua by now kuwa Mie na Hisabati sio marafiki, Biology niliipenda kwenye kuandika Essay kuhusu Maambukizo au Magonjwa(niliyajua haya kutokana na Somo la Sayansikimu kutoka Msingi), mengineyo nilikuwa sielewi(nilikuwa nasinzia). Mwalimu wetu wa Biology Kidato cha Tatu-Nne alikuwa a bit Boring au alikuwa na Mapepo(hihihi).
Yule mama alipokuwa akiingia na kufungua Mdomo "Good afternoon" mie yuleeeee Uzaramoni.....yaani macho yanakuwa mazito halafu nalala ule usingizi Mzito m paka Udenda! Nikaona aah isiwe shida bana, nikawa siingii kwenye Kipindi chake unless kuna Essay hehehehe.
Sikufanya Mitihani Miwili nayo Hisabati na Biology, kwasababu nilijua wazi sitofanikiwa kufanya vizuri na matokeo yake nikaamua ni Bora nipate alama ya Mstari(-) kuliko li-F. Wazazi wangu hawakulijua hili mpaka baada ya Kupata Majibu. Huu ulikuwa Uamuzi Mkubwa nilioufanya katika Maisha yangu nikiwa a Teenager!!
Baada ya Mitihani hiyo kupita, wanafunzi wenzangu walikuwa wakinionea huruma kuwa Mitihani Miwili ingenigharimu kwenye Points( to this day I don't know how they work out their points hihihi HISABATI).
Halafu nimeruka habari ya Mgomo wa Walimu Kidato cha Tatu, aah next week basi. Walimu pekee ambao hawakugoma Shuleni kwetu walikuwa wa Kiswahili, English na Biology.
Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments