Skip to main content

Posts

Showing posts with the label furahayandoa

Jinsi ya kurudisha Furaha Ndoani 2...

  Yafuatayo yatakusaidia kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu ikiwa mtashirikiana na kuyafanyia kazi. Yote haya mmeishawahi kuyaishi hivyo hakuna ugumu/jipya, sema tu mmezeoana so mnayachukulia kawaida, kwamba hayana "maana/umuhimu" kwa sasa.   -Wote; Acha yaliyopita huko huko yalikopita, kamwe usiayarudishe tena kwasabau tu unataka kushinda mabishano au unataka kumkumbusha mwenzio ni kiasi gani umemsamehe au namna gani alikuwa bwege hapo zamani za kale ili kumshusha na kumuumiza hisia zake(huo ni utoto).   -Wote; Unakumbuka enzi zile kabla hamjawa wazazi? Mlikuwa lovers, natambua hii inaweza kuwa ngumu hasa kwa sisi wanawake(wake)kwasababu katika haki halisi tumebadilika kiakili, kimwili na kiafya. Uzazi ni kujitolea mhanga, uzazi unakuja na trauma sio kimwili tu bali kiakili, Uzazi unabadilisha namna unamuona mumeo sio kwamba anapoteza umuhimu bali unahisi hakuhitaji tena kwasababu kuna kichanga.   Waume zetu mpo vile vile kimwili kwasababu hamkubeba mimba na hamk

Umuhimu wa Furaha ya Mke....

....wengi huchukulia suala hili juu juu tu, labda hushindwa kuelewa kwasababu Jamii (ikiongozwa na wanawake wenyewe) huwa  hailizungumzii sana kama wazungumziavyo Furaha ya Mume. Furaha ni hitaji la wote lakini nadhani kwa mwanamke ni muhimu zaidi kwasababu bila furaha kwake ni wazi watoto  na baba mtu hatokuwa na furaha. Pia furaha kwa mwanamke inahusika sana kwenye masuala ya kufanya mapenzi.....kama mwanamke hana furaha ni ama hakutakuwa na Tendo au Tendo halitokuwa la kufurahia na badala yake litakuwa ni la kumaliza haja tu kwa Mwanaume(maliza nilale arrg hihihihi). Wanaume wachache ambao wameshuhudia baba zao wakihakikisha Mama zao wanafuraha mara zote iwezekenavyo, hujitahidi na kuwa hivyo au zaidi kwa wake zao. Hawa hujua namna ya kujali  na kuheshimu hisia za mwanamke. Kwabahati mbaya sehemu kubwa ya Wanaume wamelelewa kwenye Mazingira ya kumuona Mama  ni mtu mmoja mvumilivu, mpole na muelevu.....wakati Baba Mkali na Bingwa wa kudharau. Kwamba Mama anapochoshwa n