Unawajua?
Kwanza haujambo? Anhsante sana kwa kuichagua Blog hii.
Kwa sie wa Ughaibuni (tuishio nje ya Tanzania)au wale tulioitwa Mjini kusoma au kufanya Kazi pia sisi wa Mtaani tuliamua kujaribu Fani na tukaipatia na tumefanikiwa kimtindo ndio huwa tunabeba hili limzigo.
Sawa pengine bila wewe kweli asingekuwa hapo lakini ulifanyanini hasa kwenye mafanikio yake aliyonayo hivi sasa......zaidi ya kuwa njia tu ya yeye kufika hapo na actually ukajaribu kuharibu bila mafanikio?
Kwa kawaida sisi wa Ughaibuni tukikaa sawa huwa tunapenda kusaidia wengine waje kujaribu maisha huku.
Wanafikia kwako na unawasaidia kutafuta Kazi na baada ya hapo nauli kwa miezi kadhaa halafu wanaanza kujitegemea.
Kutokana na Ughali wa Maisha Ughaibuni well UK + "kikacha" unapaswa kuchangia sehemu ya Bills.....hakuna cha bure na hakuna "nakaa kwa Anti hapa" lipa bill dadaaa au nakutimua.....hapa sio Tanzania.
Anyway.....maisha yanakuwa magumu kwa upande wako so unaongeza bidii kwenye kusoma na kufanya kazi 3 ili uweze kumudu Ada ya Chuo cha Uhakika(sio kile cha Kinaijeria alichokuombea Dada yako) £12,000 kwa mwaka sio lelemama.....unajigawa vipi.....utajijua mwenyewe.
Mpaka hapo aliekuleta hana mchango kwenye kuhama Chuo wala Ada bali wewe mwenyewe.....isitoshe kaisha kufukuza kwake na amegoma kukupa Udhamini (wa Maandishi) baada ya kuona umekuwa "kitisho" kwamba unampiku (ujanja wa kusaka mahela)......
.......wenye Nchi nao wanagoma kukuongozea Kibali kwasababu "Mdhamini" aliekuleta amegoma kukudhamini kwa Maandishi ili uendelee kusoma na hivyo kulazimika kurudi kwenu Tanzania. Na huu ndio mwisho wa "bila mimi usingekuwa hapo" kwani techically umerudi Bongo.
Haya.....unapiga mahesabu urudi kwenu mahesabu hayaleti Jawabu. Umebakiza Mwaka uvute Degirii ya Muingereza halafu upate replacement ambayo itakusaidia kupata ajira ya Kudumu(ukifanya vema).
Unachukua Risk na unabaki Nchini kwa watu bila Kibali ili umalizie Masomo.....unaishi kwa hofu na wasiwasi. Kila ukiona au kukutana na Askari unahisi wanajua huna Karatasi....mtu akibisha hodi unakimbilia auvunguni......ukiona mtu kaja kazini na amevaa kiofisa unaenda jificha Chooni....basi ni karaa tu.
Mungu anabariki unapata replacement baada ya Muda unamaliza Shule halafu KABOOM Kampuni uliyofanya nayo replacement inakudhamini na kukuombea Kibali kama Mfanya kazi wao.
Siku unarudi Tanzania baada ya miaka Tano. Hakuna anaejua uliyopitia huko utokako na kwanini hukutudi likizo.....wanakupa siku tatu uzoee halafu kila mtu anakuja na tatizo lake.....wanakuona Mkombozi....usipotoa msada kwa kiwango watakacho basi unakumbushwa "bila nanilihu usingekuwa hapo".
Najua nimekugusa au nimekusaidia uelewe upande wa pili wa Hadithi ya "bila mimi usingekuwa hapo"......
Babai.
Comments