Skip to main content

Posts

Showing posts with the label mamawanyumbani

Heri kwa Mwaka 2022, hebu tuone Past life yako...

Ni kawaida kuamini kuwa ulipigwa, tishwa, telekezwa/achwa kwa masaa kadhaa au miaka na Mama/Baba na umekua vema tu, huna shida yeyote Kisaikolojia/Kimwili/Kihisia. Unaendelea kuwapenda Wazazi wako despite the mateso walikupatia ilipokuwa kichanga, Mdogo na Kijana. Unaamini kuwa walichokifanya wazazi wako ndio kimesaidia kukufanya wewe uwe hivyo ulivyo sasa. Hakika bila wazazi wako kukulea walivyokulea usingekuwa hivi ulivyo ambavyo wewe unadhani ni "kawaida". Kukubali kuwa uliteswa/na kutengwa(rejea kipengele cha kwanza) na kuwa malezo hayo yamefabya uwe ulivyo sasa lakini una kutaa kuwa huna tatizo, tayari ni tatizo.  Nikukumbushe....Kupigwa, Kutelekezwa/achwa na kutishwa kwa awamu tofauti. Kupigwa : Ikiwa Mama/Baba kukupa maumivu ya mwili ambayo uliyachukia na kuogopa kwanini unatumia mbinu hiyo hiyo kuumiza mtoto wako? Mtoto anapofanya kosa(bado anajifunza), kwanini huchukui hatua na kumfunza/elewesha na kisha kumpa adhabu kulingana na umli wake ambayo sio kipigo.  Kwanini

Wale akina Wanangu Come First....

Hakika! wao kwanza kabla ya watu wengine baba yao included(hello Asali wa Moyo hihihihi). Hata mie nimewahi kusema/kuwaambia watu kuwa Wanangu kwanza halafu wengine na mengine ndio yanafuta. Nakumbuka nilikuwa na mwambia Mama, "nikija kuwa na mtoto, sitoruhusu mtu amshike....hata baba yake" hapo nilikuwa sijui Uchungu wa Mtoto wala Emotional connection na Bond kati ya Mimba/Mtoto na Mama. Nilihisi kuwa mtoto yupo Salama zaidi akiwa na Mama(nadhani ni Nature tu). Baada ya kuwa Mama hakika Wanangu waka wa kwanza kabla ya lolote kubwa au dogo. Maisha yangu yakazunguukwa na Wanangu na kila kitu kinachowahusu. Ikafikia mahali nikaanza kuhisi sifurahii hii "biashara" sijui "kazi" ya kuwa Mama. Ikawa too much mpaka nikasahau mimi ni nani. Nikasoma mahali (ukinipa mtihani wa Mimba, Kuzaa na kukabiliana na shida/mabadiliko ya kuwa  Mama early days baaya ya kuzaa nafaulu zaidi ya Kufaulu), maana sijawahi kusoma in my life kama nilivyosoma/ninavyoso

Kumfulia nguo sio wajibu ni msaada.

Heri ya Ijumaa! Najua umewahi kukutana au kusikia watu wakisema wanataka kufunga ndoa ili wapate watu wa kuwafulia nguo na kuwapikia er futari? Pia umewahi kuona wanaume wakimsifia mwanamke kwasababu akienda kwake lazima atamfulia nguo na hivyo mwanamke huyo anafaa kuwa mke au bado? Unakuta mtu anakasirika kabisa kwasababu nguo zake hazijafuliwa na kunyooshwa tayari kwa ajili yake akidhani kuwa hiyo shughuli ni wajibu au kazi ya Mpenzi wake(wanasahau kuwa kuna Dobi kila Mtaa). Kwa wale wanaofanya kazi nyumbani(mama wa nyumbani) kazi zao ni nyingi kuliko kazi yako nje ya nyumbani hivyo anapokufulia nguo ni msaada.....kwamba anakusaidia so usizoee ukadhani kuwa ni wajibu wake kukufuli. Kunyoosha Nguo aka kupiga Pasi huku Ughaibuni inachukuliwa kama kazi ngumu kwamba inaweka presha kwenye Miguu na uti wa Mgogo sasa imagine mkimama anaefua(kwa kuinamisha mgogo pia).....! Nina sifa nyingi kama mwanamke kwenye "shughuli" za nyumbani lakini sifa kuu ni kunyoosha Mashati na Sur