Heri ya Ijumaa!
Najua umewahi kukutana au kusikia watu wakisema wanataka kufunga ndoa ili wapate watu wa kuwafulia nguo na kuwapikia er futari?
Pia umewahi kuona wanaume wakimsifia mwanamke kwasababu akienda kwake lazima atamfulia nguo na hivyo mwanamke huyo anafaa kuwa mke au bado?
Unakuta mtu anakasirika kabisa kwasababu nguo zake hazijafuliwa na kunyooshwa tayari kwa ajili yake akidhani kuwa hiyo shughuli ni wajibu au kazi ya Mpenzi wake(wanasahau kuwa kuna Dobi kila Mtaa).
Kwa wale wanaofanya kazi nyumbani(mama wa nyumbani) kazi zao ni nyingi kuliko kazi yako nje ya nyumbani hivyo anapokufulia nguo ni msaada.....kwamba anakusaidia so usizoee ukadhani kuwa ni wajibu wake kukufuli.
Kunyoosha Nguo aka kupiga Pasi huku Ughaibuni inachukuliwa kama kazi ngumu kwamba inaweka presha kwenye Miguu na uti wa Mgogo sasa imagine mkimama anaefua(kwa kuinamisha mgogo pia).....!
Nina sifa nyingi kama mwanamke kwenye "shughuli" za nyumbani lakini sifa kuu ni kunyoosha Mashati na Suruali.....Mzee wangu alisaidia sana kwenye hili kila J'2 lazma aniite na kunionyesha namna ya kunyoosha nguo zake.
Pia alikuwa anapenda mimi nimpikie Dagaa wale wa Kigoma na Ugali....nimeanza kupika nikiwa na Miaka 8 hivi. Wachana na hili......
Stori taimu: Enzi nimeanza kutoka na Asali wa Moyo nilianza tabia ya mbaya ya kumfulia na kumnyooshea nguo (nilipogundua kuwa ni keeper bana angekuwa mpita njia wala nisingefua) na alikuwa way too busy na kazi so ili asipoteze muda kwenye usafi wa nguo na hivyo nipate muda nae nikawa namsaidia.
Basi siku moja tunaongea Simuni akanambia kuwa kanikumbuka kweli (nyumbani kwake)na alichokikumbuka zaidi ni mimi kumfulia Nguo.....aiiiii si ndio ukawa mwisho wa mimi kumfulia.
Umenona hata wa Ughaihuni wenye Mashine za kufulia bado wanaona kufua nguo ni Kazi ngumu.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Msaada na Wajibu au Kazi ni Msaada.
Babai.
Comments