Lakini bado wanavaa Nguo.....waogope sana!
Kwanza ni kwanini hasa wanaume wanapenda kufuatilia masuala ya Urembo wa Wanawake au Mavazi ambayo hayawahusu? Jibu: Wanaogopa gharama au roho mbaya bin Mfumo Dume.
Mwanamke anakuwa judged muda wote kwa maisha yake yote.....hata mimi nahukumu wanawake wenzangu na mimi mwenyewe lakini hapo hapo huwa najaribu kuelewa kwanini wapo hivyo walivyo(ukiachilia mbali Uwezo wa kifedha) kwasababu najua UANAMKE una issues zake ambazo mwanaume hawezi kuzielewa.
Kutokana na kuwa judged muonekano wa Uso/Sura ni muhimu kuliko sehemu nyingine za mwili ambazo anaweza kuziziba kwa kuvaa nguo.
Mwanamke anapendezeshwa kwa Vipodozi, Mavazi, Vito vya Thamani na Manukato. Ili mwanamke apendeze inabidi awe msafi na ili awe msafi ni lazima aitunze Ngozi yake, Kucha na Nywele......hivi vyote ni gharama.
Unawajua wale wakibaba wanaopenda independent women with natural beauty?So that they can spend their money on others while you (independent woman)pay Bills na unachuro byuti wako.....ayiiiiiii napoteza track!!!
Mwanamke anaweza kutanua matawi ya Urembo wake kulingana na miaka au Fashion na hivyo kuongezea pale anapohisi panahitaji ongezo kwa muda mfupi.
Mavazi na kujipamba au kujiremba ni moja ya sehemu muhimu sana kwenye maisha ya baadhi ya Wanawake kwani huwaongezea hali ya kujiamini na wengine wanapata furaha moyoni kwa kupata muda wa peke yake kujiangalia kwenye kioo akijifunza namna ya kuongeza urembo alionao kwa Muda.
Sasa Manabii, Mahimamu na Makasisi wa Kiume ndio imekuwa Topic siku hizi......badala ya kutangaza neno la Mungu au kuelimisha watu kuhusu Imani ya Dini husika wao wanazungumzia mavazi na Urembo wa Wanawake.
Halafu mikimama inayopenda kuwa nachuro(hawapaki hata mafuta ngozini eti sababu Waume wao wanapenda unachuro) ndio washangiliaji wakuu.
Stori time: Once aponi muda nilikuwa napenda kuwa nachuro byuti bana mpaka siku moja Konda aliponiita Uncle......"Oyaa anko ajasti kidogo basi" sababu nilikuwa nanywele fupi....halafu nimepiga shati (la shule) kubwa so Matiti hayaonekani......nililiaaa mpaka nilipofika nyumbani.
Ndio ikawa siku ya kwanza kupaka Uwanja kwenye water line na kusuka(Baba alikataza kusuka eti napoteza muda ila kilio changu kilimfanya aniruhusu kusuka) hihihihi.....I still look like my Dad's bro aka Uncle though.
Babai.
Comments