Skip to main content

Posts

Showing posts with the label natural

Juice na Soda husababisha "Homa" zisizoisha kwa Watoto....

Heri ya Mwezi mpya wa May. Mungu abariki kila jema upangalo kufanya(na-sound kama Pastor sasa eti?)! Umewahi kujiuliza kwanini Mwanao/Wanao huwa na Homa au Vikohozi visivyokwisha? Ukimpeleka Hospitali na kupima Damu na kila kitu majibu ni kuwa hana Malaria wala Typhoid (hatuna huku ila inawezekana ulipo haya Magonjwa yapo) na magonjwa Mengine ya Utotoni. Wahenga...well Bibi yangu alisema "Mwanangu kuwa Uyaone", mie nasema kuwa na Watoto ujifunze! Wazazi wengi huamini kuwa Soda  husababisha  Watoto kuchangamka kupita kiasi na pengine kukosa usingizi, baadhi huamini kuwa hufanya Watoto kuwa na tabia za ajabu(wabishi,wakahidi, hawakusikilizi, wananguvu kupita kiasi) kutokana na Soda ambayo huwafanya kuwa "high". Sasa hizo ni Soda na zina some sort of "hewa" sio, kwamaana hivyo Juice za kawaida ambazo hazina Sukari ni salama(nilidhani) tena zile ambazo unachanganya na Maji(squash) ndio Bora zaidi(nilijidanganya). Kuna wakati tulikuwa tukinunua

Wanaume wanaopenda Natural Beauty....

Lakini bado wanavaa Nguo.....waogope sana! Kwanza ni kwanini hasa wanaume wanapenda kufuatilia masuala ya Urembo wa Wanawake au Mavazi ambayo hayawahusu? Jibu: Wanaogopa gharama au roho mbaya bin Mfumo Dume. Mwanamke anakuwa judged muda wote kwa maisha yake yote.....hata mimi nahukumu wanawake wenzangu na mimi mwenyewe lakini hapo hapo huwa najaribu kuelewa kwanini wapo hivyo walivyo(ukiachilia mbali Uwezo wa kifedha) kwasababu najua UANAMKE una issues zake ambazo mwanaume hawezi kuzielewa. Kutokana na kuwa judged muonekano wa Uso/Sura ni muhimu kuliko sehemu nyingine za mwili ambazo anaweza kuziziba kwa kuvaa nguo. Mwanamke anapendezeshwa kwa Vipodozi, Mavazi, Vito vya Thamani na Manukato. Ili mwanamke apendeze inabidi awe msafi na ili awe msafi ni lazima aitunze Ngozi yake, Kucha na Nywele......hivi vyote ni gharama. Unawajua wale wakibaba wanaopenda independent women with natural beauty?So that they can spend their money on others while you (independent woman)pay Bills na