Skip to main content

Posts

Showing posts with the label wachungaji

Wanaume wanaopenda Natural Beauty....

Lakini bado wanavaa Nguo.....waogope sana! Kwanza ni kwanini hasa wanaume wanapenda kufuatilia masuala ya Urembo wa Wanawake au Mavazi ambayo hayawahusu? Jibu: Wanaogopa gharama au roho mbaya bin Mfumo Dume. Mwanamke anakuwa judged muda wote kwa maisha yake yote.....hata mimi nahukumu wanawake wenzangu na mimi mwenyewe lakini hapo hapo huwa najaribu kuelewa kwanini wapo hivyo walivyo(ukiachilia mbali Uwezo wa kifedha) kwasababu najua UANAMKE una issues zake ambazo mwanaume hawezi kuzielewa. Kutokana na kuwa judged muonekano wa Uso/Sura ni muhimu kuliko sehemu nyingine za mwili ambazo anaweza kuziziba kwa kuvaa nguo. Mwanamke anapendezeshwa kwa Vipodozi, Mavazi, Vito vya Thamani na Manukato. Ili mwanamke apendeze inabidi awe msafi na ili awe msafi ni lazima aitunze Ngozi yake, Kucha na Nywele......hivi vyote ni gharama. Unawajua wale wakibaba wanaopenda independent women with natural beauty?So that they can spend their money on others while you (independent woman)pay Bills na

Mtu wa ku-share nae matatizo yako!

Ni nani? Kuna wakati unahisi kupata mtu wa kumuambia matatizo yako ili kushusha mzigo wa mawazo.......Kama ujuavyo kulizungumzia tatizo kunakusaidia Kisaikolojia kuhisi uzito wake mabegani umepungua. Mara zote huwa tunakimbilia kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki. .....mara chache huenda kwa Viongozi wa Dini. Mzazi huwa anakusikiliza na kukupa matumaini,  ndugu na jamaa hutoa ushauri pia marafiki hujitahidi kutoka mawazo yao. Mzazi kamwe hawezi kusambaza habari za tatizo lako kwa mtu mwingine hata kama ni dada yako mpaka labda aone kuwa maisha yako yapo hatarini. Ndugu....er inategemea maana kuzaliwa baba moja na mama mmoja sio lazima mpendane....marafiki nao hupeda kufananisha matatizo ya mtu na mtu na bila kujua wanajikuta wame-share matatizo ya wenzao na wengine ni wazuri kusikiliza na kushauri kisha wanakucheka au unakuwa hadithi ya kushangaza au kuaikitisha kwao. Viongozi wa Dini wa kisasa hutumia info za matatizo yako kama mfano au shuhuda kwa Waumini wao. Wengine hutumia