Ni nani?
Kuna wakati unahisi kupata mtu wa kumuambia matatizo yako ili kushusha mzigo wa mawazo.......Kama ujuavyo kulizungumzia tatizo kunakusaidia Kisaikolojia kuhisi uzito wake mabegani umepungua.
Mara zote huwa tunakimbilia kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki. .....mara chache huenda kwa Viongozi wa Dini.
Mzazi huwa anakusikiliza na kukupa matumaini, ndugu na jamaa hutoa ushauri pia marafiki hujitahidi kutoka mawazo yao.
Mzazi kamwe hawezi kusambaza habari za tatizo lako kwa mtu mwingine hata kama ni dada yako mpaka labda aone kuwa maisha yako yapo hatarini.
Ndugu....er inategemea maana kuzaliwa baba moja na mama mmoja sio lazima mpendane....marafiki nao hupeda kufananisha matatizo ya mtu na mtu na bila kujua wanajikuta wame-share matatizo ya wenzao na wengine ni wazuri kusikiliza na kushauri kisha wanakucheka au unakuwa hadithi ya kushangaza au kuaikitisha kwao.
Viongozi wa Dini wa kisasa hutumia info za matatizo yako kama mfano au shuhuda kwa Waumini wao.
Wengine hutumia info za matatizo yako kuku-control na hivyo unajikuta unamuabudu yeye na sio Mungu wako.
Hii hukufanya upoteze control ya maisha yako na kuwa tegemezi wa kiakili kwa Kasisi sijui Nabii au Mchungaji.
Unatatizo? ni bora kulipeleka kwa mtu asiekujua na kuomba ushauri huko(najitangazia biashara iihihihihihi.)......utani pembeni.
Chagua kwa making nani wa ku-share matatizo yako......mkeo au mumeo ni salama, lakini kama matatizo yanasababishwa na mmoja wenu then Chagua kwa makini.
Babai.
Comments