Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Dini

Dini inaweza kuyumbisha Ndoa/Uhusiano wako....

Heri ya J'Nne, Kama nilivyokuahidi Wiki (mbili na Siku Moja) iliyopita (bonyeza hapa kama ulipitwa) kuwa nitakuja nikukumbushe tu ni kwa namna gani Imani yako ya Dini inaweza kuyumbisha Ndoa au Uhusiano wako. Kwa kawaida wengi hudhani kuwa mtu anapokuwa Mumini Mzuri wa Dini au "anamuogopa" Mungu ndio atakuwa muaminifu, atampenda kwa dhati, atakuwa  mkweli, hatomuumiza na mengineyo mazuri mazuri. Ukweli ni kuwa Mtu wenye Dini mara nyingi huwa mwepesi kutenda "dhambi" au yale ambayo hayaruhusiwi na Dini zao akijua kuwa atasamehewa, sio tu na Mungu bali wewe Mwenza wake unapaswa kumsamehe. "Ikiwa Mungu aliemuumba anatuambia tusamehe iweje wewe ushindwe kunisamehe". Mazoea hayo ya kutegemea kusamehewa kila unapofanya makosa ya makusudi hupelekea upande mmoja kuhisi upweke na kuondoa Amani na Furaha kwenye Uhusiano /Ndoa. Hii inaweza kupelekea kujitenga na pengine kutafuta furaha Nje ya Muungano wenu. Hilo moja. Pili, Imani yako ya Dini inak

Social Media, kama ilivyo kwa Dini ni chanzo cha Ndoa/Uhusiano wako kuyumba.

Jambo! Siku kadhaa niliuliza "kiutani" kuwa Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume  kwa Vijana(chini ya Miaka 60)Nchini Tanzania au pengine Afrika linasababishwa na nini? Wawili watatu walidai kuwa Vijana siku hizi wanapiga Mkono(kujichua) kupitiliza, binafsi nilidhani kuwa ni Mawazo kutokana na Ukosefu wa Ajira(Kipato). Hivi majuzi nikakutana na Majadiliano ya Vijana (huku niliko) wakijadili ni namna gani Instagram inawafanya washindwe kuwa watendaji wazuri Kitandani. Sio tu kwamba hawawezi ku-perform bali pia wakifanikiwa kuinuka basi mwenzo huwa mreeeefu na hawafikii mwisho. Kwa kawaida(kiuzoefu) Mzunguuko wa kwanza unaenda kwa Dakika 45 bila Mwanamke kuhisi kuchoka na bila kubadilisha Mikao(unabadili movements za Kiuno/Nyonga), na hii ni kwa Mwanamke mwenye uwezo wa "kukojoa" zaidi ya  mara moja ndani ya Mzunguuko Mmoja(Hisabati nazo zinanifuata kila mahali...I don't like them huh!). Kumbuka baada ya Mwanamke(wa kawaida, sio sie special wa Goli 3 p

How to(Jinsi ya)...kuwa Chini ya "Mumeo"....

....imekuwa kawaida kwa Wanandoa Wake kwa Wame kutafuta "jinsi ya" kufanya mambo mbali mbali ili kuifanya Ndoa kusimama Imara na kuepusha misuko-suko ya kihisia na hivyo kupelekea Ndoa kuwa Ndoano na pengine kuharibika. Hii kuwa "chini ya Mumeo" hata mie siijui na vyovyote ilivyo kamwe sitokubali kuwa "Chini" ya  Mtu yeyote achilia mbali Mwanaume ila nitakuambia ninachokijua ambacho huenda ni tofauti lakini bado kinamrudishia Mwanaume hali ya kujihisi/sikia kuwa anaheshimika/heshimiwa na Mkwe. Tatizo kubwa linalofanya Wanawake kukumbushwa au lazimishwa na Jamii kuwa ni LAZIMA wawe chini ya Wanaume (asiwe na Sauti) pale wanapoamua kufunga Ndoa ni kutokana na Imani kuwa Mwanamke anaposimama na "kujitetea" na/au kum-challenge Mwanaume basi huesabika kuwa hana Adabu, hana Heshima kwa Mwanaume husika. Ukweli ni kuwa unapokuwa kwenye Ndoa ya "ndio Bwana"  kwamba kila anachokisema Mwanaume wewe unakubali tu....huondoa Changamoto

Mtu wa ku-share nae matatizo yako!

Ni nani? Kuna wakati unahisi kupata mtu wa kumuambia matatizo yako ili kushusha mzigo wa mawazo.......Kama ujuavyo kulizungumzia tatizo kunakusaidia Kisaikolojia kuhisi uzito wake mabegani umepungua. Mara zote huwa tunakimbilia kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki. .....mara chache huenda kwa Viongozi wa Dini. Mzazi huwa anakusikiliza na kukupa matumaini,  ndugu na jamaa hutoa ushauri pia marafiki hujitahidi kutoka mawazo yao. Mzazi kamwe hawezi kusambaza habari za tatizo lako kwa mtu mwingine hata kama ni dada yako mpaka labda aone kuwa maisha yako yapo hatarini. Ndugu....er inategemea maana kuzaliwa baba moja na mama mmoja sio lazima mpendane....marafiki nao hupeda kufananisha matatizo ya mtu na mtu na bila kujua wanajikuta wame-share matatizo ya wenzao na wengine ni wazuri kusikiliza na kushauri kisha wanakucheka au unakuwa hadithi ya kushangaza au kuaikitisha kwao. Viongozi wa Dini wa kisasa hutumia info za matatizo yako kama mfano au shuhuda kwa Waumini wao. Wengine hutumia