Ni kawaida kuamini kuwa ulipigwa, tishwa, telekezwa/achwa kwa masaa kadhaa au miaka na Mama/Baba na umekua vema tu, huna shida yeyote Kisaikolojia/Kimwili/Kihisia.
Unaendelea kuwapenda Wazazi wako despite the mateso walikupatia ilipokuwa kichanga, Mdogo na Kijana. Unaamini kuwa walichokifanya wazazi wako ndio kimesaidia kukufanya wewe uwe hivyo ulivyo sasa.
Hakika bila wazazi wako kukulea walivyokulea usingekuwa hivi ulivyo ambavyo wewe unadhani ni "kawaida".
Kukubali kuwa uliteswa/na kutengwa(rejea kipengele cha kwanza) na kuwa malezo hayo yamefabya uwe ulivyo sasa lakini una kutaa kuwa huna tatizo, tayari ni tatizo.
Nikukumbushe....Kupigwa, Kutelekezwa/achwa na kutishwa kwa awamu tofauti.
Kupigwa: Ikiwa Mama/Baba kukupa maumivu ya mwili ambayo uliyachukia na kuogopa kwanini unatumia mbinu hiyo hiyo kuumiza mtoto wako?
Mtoto anapofanya kosa(bado anajifunza), kwanini huchukui hatua na kumfunza/elewesha na kisha kumpa adhabu kulingana na umli wake ambayo sio kipigo.
Kwanini badala yake unapata Hasira na kushindwa kujizuia na kisha unamalizia Hasira zako kuumiza mwanadamu mwenzio ambae hawezi kujitetea/kupigana nawe kutokana na umri wake mdogo? Ni mtoto( hilo ni tatizo).
Jiulize, ingekuwa mtu mzima mwenzio, mwenye umri na umbile kama lako, akafanya kosa alilofanya mtoto wako huyo mdogo, je ungeinuka na kuenda kumpiga ili kumfunza adabu siku nyingine asirudie kosa?
Unapoapia kuwa ukijaaliwa watoto na akafanya makosa utampiga kama ulivyopigwa wewe, ni wazi kuwa vipigo ulivyopitia bado vinakusumbua, bado una hasira na unatafuta mahali pa kwenda kumalizia.
Kabla ya watoto, pengine unapiga wadogo zako, unapiga wapenzi wako, unapiga wanyama....bado unadhani vipigo havijakuathiri?
Tafuta msaada ili upate kuwasamehe wazazi wako kwa mateso waliokupatia. Haukustahili vipigo bali Upendo, Elimu na Malezi bora.
Nikirudi nitazungumzia ile "kavae viatu twende" ukirudi Mama/Baba hayupo. Hii huwa "meme" na inachekesha sana Twita ila inaonyesha wazi imekuathiri vibaya sana.
Usikose.
Comments