Skip to main content

Posts

Showing posts with the label saikolojia

Saikolojia ni Sayansi rahisi, you need to heal...

...huwa wanamaanisha nini? ku-heal ndio kukoje wakati huna matatizo ya kiafya(kimwili)?  Kuna maneno watu wa mitandaoni wanapenda kuyatumia ili kuonekana wajuzi au wana upeo ama wana akili/wasomi(kila mtu anataka kuonekana hivyo), unakuta mtu anajieleeeeeza halafu hakuna anachoelezea, anajazia tu maneno ambayo yana-sound vizuri au kisomi ama yale "clinical" yanayotumiwa zaidi ya Wanasaikolojia(wale wenye Leseni ya kutoa Huduma hiyo baada ya kumaliza masomo na kufuzu kwa kiwango cha phD) au Madaktari wa Akili Sisi tuliosoma "Social Science" kama sehemu ya Kozi nyingine hatupaswi ku-act kama vile ni Wanasaikolojia, ni kama Sheria kuna sehemu unaijua na unaweza kuizungumzia lakini wewe sio mwanasheria, uliisoma tu kama sehemu ya Kozi yako na sio Kuisomea. Huezi amini leo ndio nimeelewa kwanini Wanasheria wa Bongo huitana "Mwanasheria Msomi". Juzi hapa nilikuwa nasikiliza PodCast(yeah them ones) kuhusu malezi ya watoto kutoka kwa "wataalamu", kukawa

Heri kwa Mwaka 2022, hebu tuone Past life yako...

Ni kawaida kuamini kuwa ulipigwa, tishwa, telekezwa/achwa kwa masaa kadhaa au miaka na Mama/Baba na umekua vema tu, huna shida yeyote Kisaikolojia/Kimwili/Kihisia. Unaendelea kuwapenda Wazazi wako despite the mateso walikupatia ilipokuwa kichanga, Mdogo na Kijana. Unaamini kuwa walichokifanya wazazi wako ndio kimesaidia kukufanya wewe uwe hivyo ulivyo sasa. Hakika bila wazazi wako kukulea walivyokulea usingekuwa hivi ulivyo ambavyo wewe unadhani ni "kawaida". Kukubali kuwa uliteswa/na kutengwa(rejea kipengele cha kwanza) na kuwa malezo hayo yamefabya uwe ulivyo sasa lakini una kutaa kuwa huna tatizo, tayari ni tatizo.  Nikukumbushe....Kupigwa, Kutelekezwa/achwa na kutishwa kwa awamu tofauti. Kupigwa : Ikiwa Mama/Baba kukupa maumivu ya mwili ambayo uliyachukia na kuogopa kwanini unatumia mbinu hiyo hiyo kuumiza mtoto wako? Mtoto anapofanya kosa(bado anajifunza), kwanini huchukui hatua na kumfunza/elewesha na kisha kumpa adhabu kulingana na umli wake ambayo sio kipigo.  Kwanini