Kuwa msafi ni tofauti na kujipenda.....Habari gani?
Mimi sio Msaaaaafi to the point nahitaji "Tiba" ya Ushauri Nasaa, lakini napenda kusafisha Bafuni/Chooni na Jikoni (nachukia kuosha vyombo though).
Maeneo au vyumba hivyo ni muhimu sana kwangu na kwa familia yangu kwasababu natumia muda mwingi zaidi.
Unapoenda Kushundi sharti utulie kwenye mazingira Masafi, haependezi kushundi(kutoa haja kubwa) huku unahofia kupata Maambukizo.
Pengine unaharakisha kutoka na kukatisha Haja yako kwasababu ya harufu ya uchafu mwingine zaidi ya Kinyesi chako.
Nahitaji kweli kuelezea kuhusu usafi wa Jikoni au Mahali unapoandalia chakula?
Kuna siku nilikabidhiwa Jiko...si unajua wale akina Wifi/Shemeji ukienda kuwatembelea wanataka wakutumikishe? Basi nikapewa Jiko....mwenye Jiko mwenyee anajipenda huyo!
Jikoni kwake sasa.....kulikuwa na uchafu worth of 3yrs akyanani nikashindwa kupika ikabidi nisafishe jiko na maeneo ya karibu. Kwenye Sinki kulikuwa na vyombo vichafu worth of 5days(Uanaume sio kigezo cha kuwa mchafu) khaa!
Anyway baada ya upishi nikaibua sababu ya kuondoka ili nisile chakula nilichopika.
Ukitaka kujua mtu Msafi au Mchafu basi mjaji kwa kuangalia Bafu/choo na Jiko au mahali anapoandalia Chakula(sio kila mtu ana jiko). Kujipenda kimwili na Mavazi sio kithibitisho cha Usafi wa mtu.
Off i go to do my dishes.....
Babai.
Comments