Skip to main content

Je ni Muhimu kurafikiana na Rafiki wa Mumeo/Mpenzio....

...just incase? Mie binafsi siwapendi Rafiki zake wote...well sio wote, wapo  ninaowapenda ila Asali wa Moyo hayupo karibu nao so nimebaki na nisio wapenda which means siwapendi WOTE!! anyway...



Siku nkaenda shiriki Semina ya Wanandoa Wachanga(mie mepita Miaka Saba so nilienda kama Mzoefu). Dunia ya leo watu wanadanganyana sana aisee. Mke wa Pastor aliedumu kwenye Ndoa kwa Miaka 28, akawa anashauri Wanawake walio Ndoani ambao hawana "uzoefu".



Mengi yalisemwa ila lililonigusa ni hili la LAZIMA na MUHIMU sana kuwa karibu na Rafiki wa Mumeo, just incase siku moja mkikorofishana na wewe ukashindwa kuongea moja kwa moja na Mumeo. Kwamba unaenda kwa Rafiki yake/zake na kuwaomba wamfikishie ujumbe....au "Ongea na mwenzio, maana mimi hanielewi" Kweli Mama Pasta? kweli kabisaa??




Huyu ni Mume wangu(najisema kimyomoyo Seminani), tulipokula Kiapo ilikuwa kati yake Yeye, Mimi na Mungu  na tuna-share kila kitu(isipokuwa Miswaki na DNA?) ikiwa kuna issue kati yetu Mama Pasta tunaiweka Issue Mezani, tunazungumza na kufikia muafaka wenyewe na Mungu wetu. Ndoa ni ya Watatu Mama Pasta, Mungu, Mume na Mke, ikitushinda tunaipeleka kwa alietufungisha ndoa, akishindwa(which is rare) basi tunarudi Nyumbani kwa Wazazi.....huko nako ikitokea Sufuri basi tutajaribu Kansela ambae ni Mtaalam na hatujui sote(hatopendelea)....duh! mpaka tufike huko Ndoa itakuwa imekwisha uwawa...mie Mwenyewe Mshauri hihihihihihi!




Hakuna Uhusiano usio yumba, sema miyumbisho inatofautiana. Jambo kubwa kwenye Ndoa yetu huenda ni dogo sana kwenye Ndoa ya Watu wengine. Mfano mie sipendi kutukanwa au kudharauliwa, sasa siku Asali wa Moyo akinitukana au kuonyesha dharau huo utakuwa Mwanzo wa Mwisho wa Ndoa yetu! hii haina Kansela wala Mfungisha ndoa....Kuvumilia? vumilia wewe....mie sijui kuvumilia matusi wala dharau.




Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa, huitaji na sio lazima kurafikiana na Rafiki wa Mumeo/Mkeo ili tu iwe rahisi ikitokea mmepishana/kosana/gombana na mwenzio. Kama ilivyo kwenye Mapenzi, Urafiki/Ukaribu na Mtu  haulazimishwi....ni ku-click au unclick!



Kwa wewe ambae hukufundwa na Bibi/Shangazi yako labda (Kama Somo la Sayansikimu, sio muhimu ila inasaidia sana Maishani) na unategemea/amini zaidi Wake wa Mapasta/Wachungaji wakushauri kutokana na "umri mkubwa" wa Ndoa zao. Tambua kuwa Umri wa Ndoa sio kielelezo cha Ndoa Imara yenye Furaha, Upendo na Amani. Wengi hubaki kwenye Ndoa kwa sababu nyingine nyingi tu ambazo hazihusiani na Maana wala Lengo la Ndoa.



Pia kumbuka kuwa Uzoefu wa Mtu sio mara zote muhimu bali Elimu. Kufundwa ilikuwa ni Elimu  ya Kijadi ya Awali ya kumuandaa Binti Kimaisha(sio kingono pekee kana wengi wanavyofanya siku hizi) atakapokwenda kuwa Mke na Mama.



Sijui nyie, lakini jinsi mnavyokuwa pamoja kwenye Ndoa ndivyo ambavyo mnajifunza zaidi kuhusu  mambo mengi kimaisha kama Pea, vilevile inafikiwa mahali mnajikuta hamuendani tena na "marafiki" zenu wa zamani ambao kila mtu "alikuja nao". Mara nyingi mnaachana na baadhi as you grow older na kutengeneza Marafiki Wapya kama Mke na Mume by the time umefikia utu Uzima mnajikuta na Marafiki wa kweli wa chache na wengi wao ni wale mliotengeneza Pamoja kama Wanandoa.




Sikutumi uwafukuze rafiki wa Mumeo ambao labda (kama mie) huwapendi, bali husihisi presha ya kujenga urafiki nao, ila ni muhimu Mumeo aelewe kuwa Humpendi fulani na fulani ili ikiwezekana apunguze kuwaleta kwenu.....you know some watu wana bad energy, ukiwaona tu energy yako na yake zina-crush(weka Smile Emoji)!!



"Waheshimu Ndugu na Rafiki wa Mumeo, lakini usirafikiane nao"-Marehemu Bibi yangu Binti Z.K.



Waulize Google for me, kwanini hatuna Emojis kwenye Blog via PC ambayo ni Google Product?

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao