....kuna Ubaya?
Baadhi ya watu wanasema SIO vema kwa Watoto wenu kuwaona mkigombana iwe ni Ugomvi Mkubwa(Pesa za Savings acc zimenda wapi?) au ule mdogo(kwa makusudi hujasafisha Bafu). Nyie huwa hamgombani? Kama hamgombani basi mmoja wenu anaishi "kisiri", ulie nae sio yeye...au mmoja wenu anamuogopa mwenzie.
Mie ni that Woman ambae nina Sauti kali/ya juu which is a shame kwasababu huwezi kujua kama ninafoka au ninaongea kawaida, sasa ukitaka kuongea kama mimi ni wazi kuwa Utakuwa unanifokea kitu ambacho kitanikera na hapo moto kuwaka...umeona? hihihihihi nataia!!
Wazazi wengi hujizuia kuanzisha "Mabishano" mapema na hivyo, husubiri mpaka Watoto watakapokwenda Kulala ndio wanaanza kubisha/fokeana. Nakumbuka wakati nakua Baba na Mama walikuwa wakifokeana Chumbani kwao(wakiamini tumelala) kumbe some of us (Mie) tulikuwa tunaenda kusimama Mlangoni na kuwasikilia ili tujue kama wanabishana/gombana au wanaongea kawaida tu na kama wanagombana, wanagombania nini?....haiwezekani iwe ni mimi tu? hehehehe.
Wakifungua Mlango ghafla najifanya nilikuwa naenda Chooni, nimepotea njia....Sikuwahi kuwaona Wazazi wangu wakifokeana/bishana/gombana mbele yetu, lakini najua kuwa walikuwa wanafokeana time to time.
Unapokuwa na Watoto(Mzazi), wakati mwingine inakuwa ngumu "kugombana" na kumaliza Ugomvi kwasababu watoto wanaingilia (huyu anakuja nakuambia anaaka Maziwa, mwingine hivi na vile)na hivyo kuharibu "ugomvi" na matokeao yake "issue" inabaki inaning'inia. Hii ni moja ya sababu ya Wazazi wengi kusubiri mpaka Watoto walale ndio "wagombane" kwa "uhuru".
Sasa, inasemekana/Aminika kuwa ni vizuri Watoto wakijifunza "real life" kutoka kwa Wazazi wao na hivyo inashauriwa kuwa ni Salama kwa Watoto kuona Baba na Mama wakibishana/gombana kwa Maneno(bila kutumia matusi), kupena nafasi ya kila mmoja wenu kujieleza ili kwa pamoja kufikia Muafaka na kumaliza tofauti zenu zilizosababisha mkwaruzane.
Pamoja na kugombana huko hakikisheni kuwa hamdhalilishani kwa kuitana majina Mabaya/Machafu au kutumia Matusi, Watoto ni kama Sponji.....wanachokisikia na kukiona kutoka kwa Wazazi (watu wa kwanza kuwaona, kuwapenda na kuwaamini) "hukinyonya" na kukitunza. Kwao itakuwa ni kawaida kwa sababu Baba na Mama hufanya hivyo pia!
Mambo vipi lakini?
Tambua kuwa Nathamini sana Muda wako hapa, Mwambie na Mwenzio. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments