Kuna baadhi ya watu wameumbwa/zaliwa kuwa Washindani na hivyo kwao ni kawaida(pia ni vizuri), mara nyingi huliweka hili wazi mwanzoni kabisa mwa Uhusiano. Wakati mwingine wewe mwenyewe unaweza tu kugundua kuwa Mpenzi wako ni Mshindani kwenye shughuli zake za Kibiashara/Kazi, Masomo, Utunzaji wa Pesa, namna anakutunza n.k. Lakini hutofikiria hata siku moja kuwa mkifunga Ndoa hatokubali wewe "umshinde" kwenye jambo lolote.
Ukiachilia mbali mtu kuzaliwa hivyo(mshindani) pia Ushindani unaweza kusababishwa na Mazingira, Uzoefu au Malezi. Kwa wale ambao wamezaliwa wachache au wengi (Mtoto wa Pili, Mtoto wa 3 au 5 kati ya watoto 8-10) au yule wa Pili kutoka Mwisho kati ya watoto zaidi ya 5(hii ni Uzoefu wangu binafsi mie sio Mtaalam).
Pengine unaweza usigundue mpaka mtakapokuwa na Watoto, ambao huibia mambo mengi sana kati ya Wewe na Mwenza wako. Kumbuka Watoto huwarudisha nyote wawili kule mlikotokea(utotoni) na hivyo kutaka kulea wanao kama ulivyolelewa wewe au tofauti na ulivyolelewa ili kuepuka Uzoefu Hasi ulionao Ukubwani....na hapa ndipo "Ushindani" huibuka.
Sasa utajuaje kama Mume/Mkeowako anakuchukulia wewe kama Mpinzani/Mshindani wake badala ya Mwenza wake?
1-Ukimnunuliza Zawadi nzuri na Ghali, basi yeye atakununulia Ghali zaidi(Wanawake huwa tunafanya makusudi ili kupata the most expensive....au ni Mimi tu?)
2-Anakukosoa kwanza kabla/balada ya kuuliza kwanini umeamua kufanya jambo fulani. Bila shaka kama Wenza mnashirikiana kwenye kila jammbo lakini kumbuka kuna Mambo mengine hutokea ghafla na hivyo kuhitaji maamuzi ya haraka na hapo kwa hapo, huwezi kumngojea Mwenza aje/apokee/rudishe Simu.
3-Anatumia Maneno ya Umoja zaidi "Mimi", "Niki", "Mwanangu" n.k....nitakupa Mifano:-
Anapowaonya Watoto..."Mimi Mzazi wako sipendi tabia mbaya badala ya Sisi Wazazi wako hatupendi tabia Mbaya".
"Hii Summer nikienda Likizo na sio Tukienda likizo. Nikimalizia ile Nyumba badala ya Tukimalizia ile Nyumba".
Mkizozana/pishana kuhusu kuadabisha Watoto hasa kama yeye ni Mfokeaji (kwamna anafoka tu hata kwa kosa la Mtoto ambalo linahitaji muongozo wake kama Mzazi)...."huyu ni Mwanangu nitamlea nitakavyo".
4-Ukikosa Nafasi fulani ya Juu Kikazi au Kielimu....haonyeshi kujali sana(anakuwa kama vile kafurahia bila kuonyesha, lakini kwa sababu ni Mwenza wako hakika utajua tu kuwa hajaumia kama ulivyoumia wewe.
5-Akigundua unafanya Jambo fulani vizuri basi hatokusaidia kamwe! ukiomba msaada atakuambia "sipendi kuingilia mambo yako" hihihihi ukweli ni kuwa hataki kufeli halafu wewe ufaulu.
6-Ukija na Wazo zuri la Kimaendeleo ama anakukatisha tamaa na baadae yeye Kulifanya au anakwambia umwachie yeye afanye Uchunguzi kwanza....hutopata majibu ya Uchunguzi kuhusu wazo lako bali atakupa Wazo lingine linalofanana na lako.
7-Kwenye Kufanya Mapenzi....unajijua upo Vizuri, lakini hata siku moja hatokusifia. Ila ukimsifia yeye anafurahia huyo halafu hakuambii kuwa kakufanyia hivyo kwa ajili yako....anasema "najua". Nikupe Mfano? napenda Mifano....:-
Sio kila siku unamfanya/mnafanyana vizuri, ila kuna zile siku unajisikia upo "Juu" na unataka kuwa "extra" unamuamulia na unauhakika kabisa kafurahia kutokana na Matokeo during na after Tendo....lakini hatokusifia ng'ooo! Ila yeye akikuamulia siku hiyo unampa sifa zake, anakujibu "i know am good" hehehehe. How rude!!
Tangu nimemalizia na mambo ya Kufanya Mapenzi basi unaonaje Post ijayo tuangalie namna ya kubana/Kaza Misuli ya Uke mara baada ya Kufanya Mapenzi Usiku tayari kwa ajili ya cha Asubuhi/Alfajiri. Sie tulio kwenye Ndoa ambao huwa hatuogi baada ya Tendo(kutunza Utamu eee)....si unajua Manii ikikaa Ukeni, Uke unakuwa "over relaxed" au tuseme "over expand(tanuka/panuka)? au hujui?...Usikose basi(Wanawake tu).
Ahsante kwa kuichagua Blog hii, nathamini na kuheshimu muda wako Hapa!
Babai.
Comments