Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ushindani

Mwenza Mshindani/Mpinzani...utamjuaje?

Kuna baadhi ya watu wameumbwa/zaliwa kuwa Washindani na hivyo kwao ni kawaida(pia ni vizuri), mara nyingi huliweka hili wazi mwanzoni kabisa mwa Uhusiano. Wakati mwingine wewe mwenyewe unaweza tu kugundua kuwa Mpenzi wako ni Mshindani kwenye shughuli zake za Kibiashara/Kazi, Masomo, Utunzaji wa Pesa, namna anakutunza n.k. Lakini hutofikiria hata siku moja kuwa mkifunga Ndoa hatokubali wewe "umshinde" kwenye jambo lolote. Ukiachilia mbali mtu kuzaliwa hivyo(mshindani) pia Ushindani unaweza kusababishwa na Mazingira, Uzoefu au Malezi. Kwa wale ambao wamezaliwa wachache au wengi (Mtoto wa  Pili, Mtoto wa 3 au 5 kati ya watoto 8-10) au yule wa Pili kutoka Mwisho kati ya watoto zaidi ya 5(hii ni Uzoefu wangu binafsi mie sio Mtaalam). Pengine unaweza usigundue mpaka mtakapokuwa na Watoto, ambao huibia mambo mengi sana kati ya Wewe na Mwenza wako. Kumbuka Watoto huwarudisha nyote wawili kule mlikotokea(utotoni) na hivyo  kutaka kulea wanao kama ulivyolelewa wewe

Mashindano.....

Ni vema kuwa Mshindani mahali pa Kazi, Shuleni au Kimichezo, kwamba ni vema kuhakikisha unakuwa juu/mbele kuliko uwezo wako. Unaweza kuwa umezaliwa hivyo(mshindani) au umejifunza kutokana na "kusukumwa" na Wazazi wako. Nimewahi kuzungumzia hili lakini niliegemea zaidi ushindani kati yako na watu wengine uwaonao kwenye Sosho media au Mtaani(au was it in my head?). Pamoja na kuwa ushindani unakusaidia kufanya vema kwenye maisha yako Kikazi, Kielimu au Kimichezo bado hali ya Ushindani au kutaka kushindana pasipo husika kunaweza kukuharibia. Ukiiendekeza hali hiyo na kuiweka kwenye kila kitu ufanyacho inaweza kuumiza watu wako muhimu kama vile mke/mume, watoto na ndugu. Kabla ya kufanya mapenzi hii inakuna kichwani "juzi na jana nilianzisha mie au nilikuwa juu.....leo zamu yake. Bila kusema unamsukuma au kumvuta mwenzio awe juu yako"? Huo ni ushindani na can put mkeo/mumeo off. Katika hali halisi....anaelianzisha ndio atakae so huyo huyo ndio awe mtendaji mkuu, k