Skip to main content

Mashindano.....


Ni vema kuwa Mshindani mahali pa Kazi, Shuleni au Kimichezo, kwamba ni vema kuhakikisha unakuwa juu/mbele kuliko uwezo wako.

Unaweza kuwa umezaliwa hivyo(mshindani) au umejifunza kutokana na "kusukumwa" na Wazazi wako.


Nimewahi kuzungumzia hili lakini niliegemea zaidi ushindani kati yako na watu wengine uwaonao kwenye Sosho media au Mtaani(au was it in my head?).


Pamoja na kuwa ushindani unakusaidia kufanya vema kwenye maisha yako Kikazi, Kielimu au Kimichezo bado hali ya Ushindani au kutaka kushindana pasipo husika kunaweza kukuharibia.


Ukiiendekeza hali hiyo na kuiweka kwenye kila kitu ufanyacho inaweza kuumiza watu wako muhimu kama vile mke/mume, watoto na ndugu.


Kabla ya kufanya mapenzi hii inakuna kichwani "juzi na jana nilianzisha mie au nilikuwa juu.....leo zamu yake. Bila kusema unamsukuma au kumvuta mwenzio awe juu yako"? Huo ni ushindani na can put mkeo/mumeo off.



Katika hali halisi....anaelianzisha ndio atakae so huyo huyo ndio awe mtendaji mkuu, kwamba amfanye mwenzie atake au awe tayati kuneng'enuka.



Pengine sio mshindani kwenye kufanya mapenzi lakini ni mshindani kwenye masuala mengine......unarudi home na kuanza kugombania TV kwa mfano...."umeshinda nyumbani siku nzima sasa ni zamu yangu".



Wengine mnapitiliza mnashindana na watoto wenu....."mmeangalia vipindi vyenu siku nzima sasa ni zamu yangu " hihihihihi well this was me nikaamua kubadilika na kuangalia Tv watoto wakilala( kama sijachoka that is).


Binafsi sio Mshindani yaani sina habari na nani kafanya nini-wapi-kwanini lakini napenda kuganya Vema na kufanikiwa hivyo naelekeza nguvu zangu kwenye Bidii zaidi ya "lazima niwe kama fulani au zaidi yake"!


Ni vema kuacha ushindani wako mahali pa Kazi au Elimu-ni na sio kuwa mshindani kwenye kila kitu na hivyo kuharibu au kuondoa maana ya Familia/Ndoa yenye furaha.

Nakupenda kwa kuitembelea Blog hii leo.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao