...muendelezo wa Post ya jana, kama hujaiona bofya hapa. Najua ungependa kujua namna ya kumheshimu Mumeo zaidi badala ya kuwa Chini yake si eti? Kama ujuavyo sote tumepetia Mazingira/Malezi/Makuzi tofauti na hivyo hatufanani Kitabia, hivyo basi Kuheshimu Mume nijuavyo mie huenda ni tofauti na ujuavyo wewe.,...sasa labda chukua ambalo ulikuwa hulijui na ongezea kwenye yale uyajuayo? au acha kama yalivyo ila ukiweza share yako na mie "niangalizie".
Kumbuka Heshima ni muhimu kwa pande zote mbili lakini leo tunaegemea kwa Mwanaume kwasababu mimi ni eerrrr Mwanamke? also Topic ilikuwa Mwanamke kuwa Chini ya Mwanaume? Sasa kama tumeelewana hapo, twenzetu;
Muachie maamuzi Makubwa-Hata kama Kipato chako ni Kikubwa mara Nane kuliko chake, Sio unajiamulia tu kununua Nyumba au kupeleka Watoto Private School kwa mfano..... kwasababu tu unaweza. Mpe Mumeo nafasi na mjadiliane. Unaweza kuweka Mezani aina/sehemu 3 za Shule/Nyumba na kisha muache yeye afanye Uamuzi wa Mwisho kisha mpe-support. Baadhi ya Wanaume ni wazito kwenye Utendaji na kuna namna ya kukabiliana na hili, ila sio kufanya maamuzi Makubwa kisha unampa ripoti ya nini ulichofanya.
Salamu-Kwasababu tu mmelala pamoja na hukuhisi akigalauka Usiku haina maana alilala vizuri na kumbuka usiku ni Mrefu...pia hamkuwa wote Ndotoni. Kama mlivyokuwa enzi zile kabla hamjafunga Ndoa eeeh! umeamkae leo mpenzi....well sio lazima useme hivyo, Mambo?, Umeamke? Upo okay? etc! Pia katikati ya siku akiwa kwenye mishughuliko yake na atakapowasili Nyumbani.
Shukuru-Pamoja na Usawa wenu bado Mwanaume huwa na Presha kubwa ya kulinda na kutunza Familia yake. Onyesha shukurani kwake kwa yote afanyao kama "mwanaume". Kushukuru hapa kupo kwa aina tofauti sio lazima useme "ahsante Mume wangu kwa kuwa mwanaume wa nguvu/kweli" bali unaweza kusema zaidi kwa vitendo(nitaandika Post inayojitegemea kwenye hili...nikumbushe au vipi?).
Pia ni muhimu kumshukuru kwa lolote analokufanyia hata kama ni dogo, Mfano kaamka leo na kasafisha vyombo....mwambie ahsante. pengine kawahi kuamka na kuwaandalia watoto Kifungua kinywa lakini kaenda tofauti na utaratibu uliowawekea watoto na hivyo kuharibu utaratibu wa siku nzima.....mshukuru tu hivyo hivyo.....hihihihihi!
Jijali/Jipende/Jirembe-Sijui wale "napenda Nachuro" nafasi yao ipo wapi Mbinguni? ila ni muhimu sana kujipendezesha na kuonyesha kuwa unajijali kwa ajili ya Mumeo. Ikiwa wote ni Wafanyakazi nje ya Nyumbani basi Mkimama jitahidi kuwa unawahi nyumbani mapema kabla yake ili upate muda wa "kujiweka sawa" kwa ajili yake. Kupendeza kwako sio tu kutakufanya ujisikie Vizuri kama Mwanamke pia ni wazi kuwa kutaonekana kwa Watu wengine na hivyo Mumeo kuonekana kuwa anajua kutunza Mkewe.....hii kwa baadhi ni Heshima kwao!
Uliza kabla ya Kukosoa-Hasa kama Mnawatoto au Mnabiashara pamoja au vyote. Kuna sababu kwanini kafanya alichokifanya hivyo basi kabla ya kuanza kumkosoa ni vema kuuliza kwa upole kwanini kitu fulani kimefanyika ili upate kuelewa na hivyo kutafuta ufumbuzi kwa pamoja. Epuka kukosoa-kosoa mara kwa mara!
Usimseme vibaya/Mshushua-Mbele ya rafiki zenu, kuna wakati Mumeo anaweza kuteleza/lopoka mbele ya Rafiki zenu kwenye Party au mkusanyiko wowote.....lolote lililomtoka muunge mkono na kuwa upande wake(bila kusema neno). ikiwezekana kuwa sharp ku-justfy (muokoe kutoka kwenye kujiabisha).....mkifika nyumbani ndio umuweke sawa. usimuweke sawa mbele ya watu wengine no matter how close you are with those watu.
Usilalamike au kunong'ona-Kama kuna kitu Kikubwa kafanya hakijakupendeza, tafuta muda weka issue Mezani muijadili kwa upole na Upendo. Vitu vidogo vidogo kama vile Kunya/Kojoa pembeni ya choo(yes some Mumes still do that), kutosafisha bafu baada ya kuoga au kutoweka kitu mahali pake...sio kwamba anafanya hivi kwa sababu wewe ni "kazi ya Mwanamke" bali hivi vitu sio Muhimu kiviile kwake(inategemea na Malezi). So rekebisha na move on au mwambie moja kwa moja ili aache habits hizo.
Mhusishe kwenye Utaratibu wa Siku wa Watoto-Mama ndio huwa Mstari wa mbele kuweka Sheria, Kuweka Ratiba, Kuweka utaratibu n.k. katika harakati za Malezi na kurahisisha Maisha, mara nyingi Baba huwa Kazini akifanya yake ya Kibaba ili kuweza kutunza familia yake. Hivyo kupitwa na yote uliyoyaweka ambayo wewe na Watoto mnayafuata ili kurahisisha Maisha ya kila siku ni rahisi. sasa ni muhimu kumhusisha Baba ili ajue yote yanayoendelea. Sio mara zote atapatia lakini itakuwa rahisi kumuweka sawa ikiwa tayari ulikwisha muelezea utararibu wa siku wa watoto. Wakati mwingine watoto watamwambia "Mama hafanyi hivyo, Baba umekosea"!!
Muandalie Chakula aka "umtengee" mara nyingi, natambua kuna zile siku ambazo unakuwa hoi na yeye anaelewa kuwa umejichokea na hivyo anaingia mwenyewe Jikoni na Kujipakulia. lakini jitahidi kuweka chakula tayari kwa ajili yake.
Usikivu-Mumeo anapozungumzia issue muhimu ya kifamilia (hata kama mwanafamilia wake humpendi) au pengine adha alizokutana nazo Kazini, msikilize kwa makini bila kumkatisha au kuonyesha kuwa haupo inteested.
Usimuingilie kwenye Muda wake na Watoto-Hii ni ngumu(nakwambia kama Mama), lakini ni lazima ujifunze kutoingilia afanyacho Mumeo kwa Watoto wenu so long hakihatarishi Maisha yao Kihisia au Kisaikolojia...maana some Babaz nao huwaga wapuuzi, hupenda kuogopwa rather than kuheshimuwa na watoto. wanadhani ni sifa!
Uelevu kwenye "Hadithi" zake- Inaweza kuwa Siasa, Uchumi n.k....chochote ambacho kinam-interest. Jitahidi kumuelewa na ikitokea huelewi mahali ni vema kuuliza kabla hajaendelea ili arudie tena kuliko kujifanya umeelewa halafu uulize tena mbeleni wakati alichokuwa akikielezea kimekaribia Mwisho....hii hukatisha tamaa na kuonyesha kwamba ulikuwa hausikilizi na hivyo kuua "stimu" ya Hadithi.
Omba Ushauri na wake-Ikiwa kunajambo ungependa kulifanya na huna uhakika, kabla ya kuomba ushaurii kwa shoga zako au Mama/ndugu zako....Muombe yeye kwanza!
Epuka kulimbikiza Makosa ili Kumsuta- Mwanaume kama Mwanaume, usipoliweka wazi Kosa lake linapojitokeza basi ndio imetoka hiyo....ama hajui kama amekukosea au anasahau. Sasa ukitokea Mzozo na wewe ukayaingiza yote hayo kwake inakuwa kama vile unamsuta kwa Makosa ambayo hayajui(yapo kichwani mwako).
Usiingilie Ugomvi wake- Kabla Era ya Sosho Midia haijajulikana wengine hapa tulifundwa kuwa tusiingilie Ugomvi kati ya Mume na Ndugu zake, na badala yake kuwa "sikio" na usikilize....akiomba ushuari basi shauri kwa makini na hakikisha ushauri wako haukandamizi upande wa Pili ambao ni Ndugu zake. Kuwa upande wake lakini pia kuwa Fair, kwani hao ni Ndugu na wewe ni Mwanamke tu(Ouch)!!
Sasa Era hii watu na wake zao wanafuatana humo Sosho Midiani, time to time Mume anaweza kupishana na Mtu/watu.....ikawa ngumu kwako kama Mke kushuhudia Mumeo akiwekwa Konani. Jitahidi usiingilie, mwache amalize Ugomvi wake mwenyewe!
Kwa leo wacha niishie hapa, Tambua nathamini Muda wako hapa na Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai!
Comments