Kwa maCeleb Ego hujionyesha wazi kwenye mahojiano ya moja kwa moja. Baadhi wanadhani kuwa ni wao tu ndio wanazo hizo Ego, nitakupa mfano na pengine kukusaidia(kama hujui) kuitambua kutoka kwa Mwenza wako.
Kwa mimi na wewe Ego zetu hujitokeza zaidi pale tunapogombana. Ndoani/Mahusiano huwa tunagombana sana eti? Wakati mwingine ugomvi unakuwa hauna hata maana.
Ujue kuna ile kugombana kwasababu mmoja wenu kafanya kosa kubwa kama vile umegundua kuwa amekuwa akipeleka Pesa mahali ambapo hupajui! Kwa mfano. Sio kwanini hakupokea simu?!!
Na ikiwa mnawatoto basi mnaweza kugombana kwasababu mmoja wenu anahisi kuwa anaingiliwa kwenye kona yake ya malezi(wanaume) au mwingine(sisi wakimama) kuhisi kuwa watoto wanaonewa au mwenzio hatoi muda kuwaelewa watoto na badala yake anatanguliza kufoka (hasira) kwa watoto.
Katika hali halisi kama mmoja wenu anawakilisha linalomkwaza kwa namna ya kawaida(kukereka bila hasira/kufoka) na mwingine kusikiliza hakutokuwa na ugomvi. Inaitwa MAWASILIANO/KUWASILIANA.
Lakini kwa sababu ya Ego kubwa (kujiamini kupita kiasi/kiburi) au ndogo(kutojiamini/kujishtukia)ya wenzetu wa Jinsia ya Kiume kunasababisha issue ndogo kuwa kubwa.
Kwanini inakuwa kubwa? Kwasababu wanawake tunapenda kuongea na kuelezea kila kitu(mie), wakati wenzetu hawapendi kusikiliza na matokeo yake utaambiwa "yameisha, sitaki kusikia/ongelea hii issue tena" wakati hatujamaliza. Au anakuvuta na kukubusu au kufanya Mapenzi matamu ya ki-Ego hehehehe ili tu usiendelee kumwaga manoleji.
Sasa kwasababu hujamaliza ni wazi kuwa issue itakuwa inaning'inia na itakukera kwa muda wa siku 3 kama sio Wiki nzima....kwanini amekukatisha? Kwanini hataki kuimaliza issue na mfikie mafaka? Well sababu ya Ego yake.
Kwa Weusi Ego huenda juu kupita maana ya juu kwasababu wanaume wa Kiafrika hawapendi kufunzwa au kuelekezwa na Wanawakee......ikiwa mwanamke anaelekeza basi utaambiwa huna heshima au unajifanya unajua wakati hujui kitu(kwasababu tu wewe ni mkimama).
Kisayansi, Wanawake tunakua kiakili haraka kuliko wenzetu na wepesi kujifunza na wazuri kutunza info (za maana na makorokoco)kuliko wanaume. Pia tunafunzwa au tunapata uzoefu wa kimaisha kama sehemu ya kufunzwa, tofauti na wanaume ambao huachwa wajifunze wenyewe. Hivyo ukweli ni kuwa sisi tuna knowledge kuu zaidi ya wanaume(inategemea na umri/elimu though).
Sasa unafanya nini ikitokea Ego ya mwenza wako ipo juu zaidi ya Masikio yake? Well akianza kuja juu wewe Msikilize halafu dharau. Siku akitulia ibua issue kwa upole na muimalize.
Ukijibu ni wazi mtakuwa mnajibizana na hakutokuwa na mtu anaemsikiliza mwenzie na matokeo yake mnaishia kuwa na mahasira ambayo hawasaidii.
Sasa Imagine mmoja wenu anarudisha namba(anakufa) baada ya ugomvi wa kijinga unaohusisha ego zaidi ya Uelevu? Anakufa bila muafaka......Ze hatia sasa!
Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments