Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ego

Pale unapokuwa Mke mwema....

....halafu unaonekana sio mwanamke "kamili", kwanini? kwasababu hulalamini-lalamiki pale mumeo anapoacha bafu chafu baada ya kuoga au pengine anachelewa kuamka na kuacha kitanda kipo shagala bagala....(hizi sio kazi za mwanamke ni usafi), huombi-ombi pesa ya manunuzi, Vipodozi wala Salon. Inawezekana upo hivyo kutokana na Malezi/mafunzo uliyopitia au huenda umejifunza kupitia Blogs, maana Siku hizi kuna kila aina ya maelezo yanayotuelekeza namna ya kuwa  Wake(na waume) wema, mengine ni mazuri na mengine yanapotosha.....Akili kumkichwa unapoamua kuchukua na  kujaribu ulichokisoma! Ulalamishi na kutaka jambo/kitu kifanyike pale tunapotaka  ndio  inatufanya wanawake kuwa wanawake (ni sehemu ya uanamke), sasa hayo yakikosekana inakuwa kama vile Mumeo ameoa  mwanaume mwenzie ahahahaha. I mean sawa kujitegemea kiuchumi na kuepuka ulalamishi.....lakini pia tukumbuke kuwa baadhi ya Wanaume hupenda Changamoto Ndoani (sio za kugombana na muumizana mioyo/hisia)! Nat

Knowledge vs Ego....

Kwa maCeleb Ego hujionyesha wazi kwenye mahojiano ya moja kwa moja. Baadhi wanadhani kuwa ni wao tu ndio wanazo hizo Ego, nitakupa mfano na pengine kukusaidia(kama hujui) kuitambua kutoka kwa Mwenza wako. Kwa mimi na wewe Ego zetu hujitokeza zaidi pale tunapogombana. Ndoani/Mahusiano huwa tunagombana sana eti? Wakati mwingine ugomvi unakuwa hauna hata maana. Ujue kuna ile kugombana kwasababu mmoja wenu kafanya kosa kubwa kama vile umegundua kuwa amekuwa akipeleka Pesa mahali ambapo hupajui! Kwa mfano. Sio kwanini hakupokea simu?!! Na ikiwa mnawatoto basi mnaweza kugombana kwasababu mmoja wenu anahisi kuwa anaingiliwa kwenye kona yake ya malezi(wanaume) au mwingine(sisi wakimama) kuhisi kuwa watoto wanaonewa au mwenzio hatoi muda kuwaelewa watoto na badala yake anatanguliza kufoka (hasira) kwa watoto. Katika hali halisi kama mmoja wenu anawakilisha linalomkwaza kwa namna ya kawaida(kukereka bila hasira/kufoka) na mwingine kusikiliza hakutokuwa na ugomvi. Inaitwa MAWASILIANO/K