.....hapa lazma nivabe! Lakini kwasababu napenda kuchangia "knowledge" sio mbaya nikikuelezea nilichojifunza. Inawezekana kabisa hukubaliani na ninachotaka kuandika, basi angalau nipe nafasi na unisikilize(soma na share....ahsante).
Unajua pale unaanzisha Topic halafu watu wanaivamia na kuaanza Malumbano (ya busara) halafu wewe upo pembeni unafurahia huku unachukua "Material", basi ndivyo ilivyokuwa.
Wengi tunaamini(mie mmoja wao mpaka Wiki Majuzi) kuwa Mwanume Rijal/Kamilii ni yule mwenye Uwezo wa Kusimamisha Uume kwa muda Mrefu au mwenye uwezo wa Kusimama na kufanya mapenzi na kufanikiwa kummimba mwanamke.
Baadhi hudhani kuwa Wasenge sio Marijali kwasababu hawapendi wanawake aka hawawezi kuingia ukeni sababu hawawezi kuinuka(Hanithi).....kama Kusimamisha kwa muda mrefu ni Urijali basi hawa majamaa ni MARIJALI haswa!! Achana na hili.
Sehemu ndogo wanaamini kuwa kama Mwanaume ni Rijali mwanamke mmoja hamtoshi....daah! Ujinga Mzigo. Hawa wanachanganya Uwezo mkubwa wa Kungonoka na Uwezo wa Kusimamisha in which vyote sio Urijali.
Urijali ni Uwezo wa Mwanaume kufanya mambo ya Kiume kwa maana ya Kiume, Mwanaume Rijali anajua Majukumu yake na anaheshimu nafasi yake kama mwanaume kwenye Familia yake, haogopi kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya watu muhimu maishani mwake(Mke na watoto), yupo tayari kufanya lolote kwa yule ampendae, sio rahisi kushawishika, anajua kuushinda Moyo/tamaa zake, anajua thamani ya mwanamke(sababu kazaliwa na mwanamke).
Sasa Urijali sio Uwezo wa kufanya Ngono kwa Muda mrefu, Kuzaa watoto wengi kila kona ya Mtaa au kufanya Ngono mara nyingi kwa Siku na sio ile hali ya kumtamani mwanamke au kutamani utupu wake. Kumbe Urijali hauna uhusiano na Uwezo wa Kusimamisha na kutoa Manii.
Urijali ni kuwa Mwanaume Kamili/wa Kweli. Haya ndio nimejifunza kutoka kwa Wanaume Watu wazima wa Kitanzania nilipokuwa Likizo. Iwe hukubaliani au unakubaliana nao. Tambua umekuwa "Inspayadi" hivyo basi nenda kaanzishe Blog uweke Maoni yako....hah!
Ahsante kwa kuchagua Blog hii.
Babai.
Comments