Haiyaaa!
Kiangazi Kimeisha na Mvua ime-cotton fire, hii sio sababu ya wewe kuacha kuoga. Usafi wa Mwili ni muhimu kama vilivyo vitu vingine Maishani. Lakini je wewe unaoga mara ngapi kwa Siku? na je kuna ulazima wa kuoga zaidi ya mara moja kwa Siku?
Wanawake tunapewa/peana PRESHA kuoga-oga mara nyingi na tunaambiwa tusipooga tunatoa harufu kwa sababu ya Maumbile yetu, lakini wanasahau kuwa kunakosababisha harufu sio mwili as in Ngozi, bali kwapa na kunako(Nyeti) ambazo hata wanaume wanazo na zinatema harufu pia ikiwa hazitaoshwa.
Sasa nikianzia mwisho, hakika kuna ulazima wa kuoga zaidi ya mara Moja kwa siku, Inategemea unafanya kazi gani na wapi, unatumia Usafiri gani(kubanana kwenye daladala/train hakika unabeba wadudu) na bila kusahau hali ya hewa. Ikiwa unafanya kazi Hospitali(una deal na maambukizo), unaishi mahali penye joto sana au kazi yako inakufanya utoke jasho sana mpaka unanata basi wewe oga mara zote unazohitaji.
Kitibabu tunapaswa kuoga angalau mara Nne kwa Wiki, hii ni kuisaidia Ngozi kutunza Mafuta yake asili na hivyo kuwa na afya njema. Pia inasemekana kuwa Kuoga mara nyingi kwa siku kwa kutumia Sabuni kunaongeza uharibifu wa Ngozi kutokana na matumizi ya Sabuni(Kemikali).
Nikijibu swali la pili, Mimi naoga Mara moja kwa siku(siku saba za Wiki), na ni Usiku tu (nitakuambia kwanini as we go along)......nimezaliwa na Kukulia Dar es Salaam hivyo kuoga mara TATU/Nne kwasiku ilikuwa ni kawaida(baada ya Kubalehe). Kabla ya hapo nilikuwa naoga/ogeshwa Jioni tu.
Nimeamua kuoga Mara moja kwa Siku baada ya Kuwa mama(sina Muda)......unakumbuka Enzi zile(au ni mie tu) ukiamka asubuhi unasafisha Kinywa, Uso, kwapa na Sirini(kuchamba) halafu unamalizia kulowesha Miguu ili kuwezesha Mafuta ya Rays ku-apply vema? Hii ilisaidia kuokoa Muda wa Baba/Mama (hasa kama mmpo wengi) na wote mnatakiwa kutoka kwenda Shule pale Baba/Mama anapotoka kwenda Kazini au kabla.
Sababu za Mimi kuoga Usiku tu(kama unajali):-
1)-Ni muhimu kuosha matatizo na vumbi/mioshi(hali ya hewa Chafu) yote ya siku nzima kabla ya kwenda kulala.
2)-Ngozi inajitengeneza/tibu vizuri ikiwa safi na unapokuwa umelala.
3)-Ni muhimu kuneng'enuka mwili ukiwa msafi/fresh(una harufu yake asilia).
Mara zote mwili (weka pembeni Uso, Kwapa na Nyeti) huwa hauchafuki kama unavyofikiria, hata unapokuwa Hedhini(mwanamke) au umefanya Ngono(wake kwa waume) huitaji kuoga Mwili mzima isipokuwa unasafisha pale panapohitaji kusafishwa.
Tambua nathamini ushirikiano wako, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Nikuache sasa, Babai.
Comments