Skip to main content

Posts

Showing posts with the label usiku

Kuoga Usiku Vs Asubuhi/Mchana!

Haiyaaa! Kiangazi Kimeisha na Mvua ime-cotton fire, hii sio sababu ya wewe kuacha kuoga. Usafi wa Mwili ni muhimu kama vilivyo vitu vingine Maishani. Lakini je wewe unaoga mara ngapi kwa Siku? na je kuna ulazima wa kuoga zaidi ya mara moja kwa Siku? Wanawake tunapewa/peana PRESHA kuoga-oga  mara nyingi na tunaambiwa tusipooga tunatoa harufu kwa sababu ya Maumbile yetu, lakini wanasahau kuwa kunakosababisha harufu sio mwili as in Ngozi, bali kwapa na kunako(Nyeti) ambazo hata wanaume wanazo na zinatema harufu pia ikiwa hazitaoshwa. Sasa nikianzia mwisho, hakika kuna ulazima wa kuoga zaidi ya mara Moja kwa siku, Inategemea unafanya kazi gani na wapi, unatumia Usafiri gani(kubanana  kwenye daladala/train hakika unabeba wadudu) na bila kusahau hali ya hewa. Ikiwa unafanya kazi Hospitali(una deal na maambukizo), unaishi mahali penye joto sana au kazi yako inakufanya utoke jasho sana mpaka unanata basi wewe oga mara zote unazohitaji. Kitibabu tunapaswa kuoga angalau