Natumaini Post hii itakukuta ukiwa Mzima wa afya.
Kama nilivyoahidi, leo nitakuelezea utaratibu wangu uliosababisha nywele(Relaxed) zangu kurudia Afya yake baada ya kuzipoteza na kupata "upara" wa muda.
Jikoni kuna mwanga asilia, sihifadhi Bidhaa hizi Jikoni....hihihi! |
Ukiachilia mbali kuongeza aina ya Mboga iitwayo Kale kwenye Mlo wangu wa kila siku na kula Mayai 2-3 kila asubuhi. Bidhaa hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kuzuia Nywele zangu kuendelea kung'oka/anguka baada ya Kujifungua.
Utaratibu wangu Rahisi.
Kila Siku: Napaka Cantu Shea Butter kila siku asubuhi na Jioni na baada ya kupaka Cantu huwa na-"seal" na Mafuta asilia ya Sweet Almond.
Kila Wiki: Huosha na Deep Condition Nywele zangu mara Moja (kila Ijumaa/JumaMosi) na huwa natumia Cream of Nature shampoo. Baada ya hapo nafanya deep condition kwa kutumia Vitale Mayonaise ambayo huwa nachanganya na Hello hydration (haipo pichani) na aina 2 za Mafuta asilia ambayo ni Nyoyo(Costor oil ) na Olive(extra virgin.). Huwa nakaa na mchanganyiko huo kwa Dakika 45-Saa Moja nikiwa kwenye Steamer.
Nasuuza kisha napaka Keracare Natural texures na Keracare normal leave ins na kisha kukausha nywele kwa kutumia Blow dryer(nitaweka Picha ya Tools kwenye post nyingine).
Kila baada ya Mwezi: Naosha(deep clense/clarify) Nywele kuondoa uchafu uliosababishwa na bidhaa nilizokuwa natumia kwa mwezi husika na hapa huwa natumia Vitale Breeze Shampoo na kutumia Mchanganyiko wa Deep conditioner nitumiao Kila Wiki.
Kila baada ya Mwezi na nusu: Huwa nafanya "Protein treatment" kwa kutumia Aphogee step 2(fuata maelekezo kwa makini) na baada ya hapo huwa natumia Keracare Humecto ili kuepusha ukavu/ugumu kwenye nywele.
Kila baada ya Miezi 3: Huwa nahina(kupaka Hina kwenye Nywele). Hina nitumiayo ni ile asilia moja kwa moja kutoka Mtini(naagiza kutoka Tanzania). Huwa nachanganya na Chai ya joto kiasi, kisha naiacha kwa masaa 12 then naipaka na kuiacha kwenye Nywele kwa masaa 3 hadi 5.
Baada ya hapo naosha na kupaka Keracare Humecto conditioner ili Nywele zisiwe kavu/ngumu. Hina inaongea "nguvu" kwenye nywele kama Protein na pia huzilainisha ila mie naitumia kwa ajili ya Rangi kwani nywele zangu si Nyeusi vya kutosha na sipendi Weusi wa kutosha hihihihihi so yeah kale kawekundu ka Hina kanaweka u-brown-ish Nyweleni.
Hakikisha kuna nafasi ya kutosha kati ya Protein treatment na Hina Treatment. Mie huwa naweka Relaxer kila baada ya wiki 10 na Miezi Mitatu(Wiki 12) na wiki mbili au Tatu baadae ndio nafanya Hina treatment.
Kama hujawahi kujifungua na kupoteza nywele au Nywele sio muhimu kwako basi huwezi kujua umuhimu wa Post hii. Back then hakukuwa na Post nyingi online, nilihangaika mno kutafuta maelezo ya nini cha kufanya na namna ya kufanya (sikuwahi kupatwa na issue hii). Naweka uzoefu wangu ili Mwanamke mwingine mwenye tatizo hili asihangaike sana kama mimi.
Ijumaa (Christmas day) hii nitanyoosha Nywele zangu na kuchukua picha na kulinganisha na ya 2014 ili niweze uweze kuona tofauti na "upara" wangu wa muda.....hii itakuwa kwenye Post ya Vifaa vya Umeme nitumiavyo kutibu na kuremba Nywele zangu.
Nathamini na kuheshimu Muda wako hapa, ahsante sana kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments