Yeboyebo hihihihi bado mnatumia hili neno? Wasukuma wa Shinyanga (enzi za Usichana) walikuwa wakisema Yebaaa as in Yeah....."Wananchi Mpo?" "tupo tupo kabisa kwa Jeuri ya Chama yee yee yeebaa". Twende kwenye Krismas sasa.
Kwa kawaida mie huwa siandiki kuendana na Nyakati lakini Mwaka huu ni tofauti kwa sababu Waanangu has huyu Mkubwa kanifanya nianze kuipenda na kuifurahia Krismas tena. Miaka 3 nyuma alikuwa Mdogo so hakujali mapambo wala Santa, Mwaka huu anakaribia miaka 5 na yupo Shule ambako wanafunzwa kama sehemu ya Utamaduni.
Babuu akaandika(makorokocho) Barua yake kwa Santa akiorodhesha zawadi aitakayo na akatengeneza na Bahasha kisha kuiweka na kumpa Baba yake akaipost(which he did, huruma kwa postman mkusanya barua hihihi). Sasa kila leo anamzungumzia Santa na kudai atakuwa extra nice na kunisaidia kusafisha(anaacha toys kila kahali) ili Santa asibadili mawazo na hivyo yeye kukosa Zawadi siku ya Krismasi.
Walipoanza kupamba Shuleni kwako akaja hima nyumbani akitaka na sisi tusimamishe Mmkrismasi(wa nailoni, tunaamini katika kutunza nature hihihihi usitujaji).....kwa maana hiyo humu ndani kuna Mapambo ya Krismasi tangu Novemba 20.....uzuri baridi sio kali sana,vinginevyo ningelalamika wanamaliza Umeme kwa kuwasha mataa 1st thing wakiamka mpaka wanapoenda kulala,....12hrs ya vimulimuli. Anyway, ukiangalia wanavyofurahia na kuhesabu siku zilizobaki kabla ya Krisimasi kila siku inakupa furaha na kusahau "Gharama" ya Umeme.
Niliacha kusheherekea Krismasi baada ya kujua maana yake ambayo ni zaidi ya Mavazi, kula na kusaza na kisha kupewa pesa (zawadi ya xmass) na kila Mgeni aliekuja kula kwenu. Kwa kifupi ni kwamba sikuwa mtoto tena na vitu hivyo havikuwa na umuhimu tena kwangu.
Ila mwaka huu ni tofauti kabisa, na itakuwa hivyo mpaka Babuu na Kibibi watakapokuwa watu wazima, may be 21yrs later?.....ntakuwa full of Botox na fillers(kutakuwa na better mbadala i guess).
Nakutakia wewe msomaji wangu na familia yako Heri ya Krismas. Furahia wakati wako na kumbuka kuwa Muangalifu kwani siku 7 kabla mwaka haujaisha ni Nyingi zaidi ya kuwa Januari nakuingojea December(sijui umenielewa?).
Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments