Skip to main content

Posts

Showing posts with the label rahayawatoto

Kristmas mwaka huu ni tofauti....

Yeboyebo hihihihi bado mnatumia hili neno? Wasukuma wa Shinyanga (enzi za Usichana) walikuwa wakisema Yebaaa as in Yeah....."Wananchi Mpo?" "tupo tupo kabisa kwa Jeuri ya Chama yee yee yeebaa". Twende kwenye Krismas sasa. Kwa kawaida mie huwa siandiki kuendana na Nyakati lakini Mwaka huu ni tofauti kwa sababu Waanangu has huyu Mkubwa kanifanya nianze kuipenda na kuifurahia Krismas tena. Miaka 3 nyuma alikuwa Mdogo so hakujali mapambo wala Santa, Mwaka huu anakaribia  miaka 5 na yupo Shule ambako wanafunzwa kama sehemu ya Utamaduni. Babuu akaandika(makorokocho) Barua yake kwa Santa akiorodhesha zawadi aitakayo na akatengeneza na Bahasha kisha kuiweka na kumpa Baba yake akaipost(which he did, huruma kwa postman mkusanya barua hihihi). Sasa kila leo anamzungumzia Santa na kudai atakuwa extra nice na kunisaidia kusafisha(anaacha toys kila kahali) ili Santa asibadili mawazo na hivyo yeye kukosa Zawadi siku ya Krismasi. Walipoanza kupamba Shuleni kwako akaja